Mama wa Kristo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani wa kwanza kuhusu Bikira Maria na Mwanae, katika Handaki la Priscilla, Roma, katikati ya karne ya 2.

Mama wa Kristo (kwa Kigiriki: Χριστοτόκος, Christotokos, yaani Mzazi wa Kristo, kwa Kiingereza: Christ-bearer[1]) ni sifa mojawapo ya Bikira Maria, mama wa Yesu Kristo, inayopendelewa na Wakristo wa Kanisa la Waashuru la Mashariki na wengineo ambao hawapendi dogma ya Mtaguso wa Efeso (431) la kwamba Maria anastahili kuitwa Mama wa Mungu kwa sababu alimzaa Mungu Mwana kama binadamu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Hall, Christopher Alan (2002). Learning Theology With the Church Fathers. InterVarsity Press. ku. 8–9. ISBN 9780830826865. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mama wa Kristo kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.