Bikira Maria wa Mateso

Bikira Maria wa Mateso ni jina mojawapo linalotumika kumheshimu mama wa Yesu kama mshiriki mwaminifu na wa dhati wa mateso na kifo cha Mwanae msalabani.
Liturujia ya Kanisa la Kilatini inaadhimisha kumbukumbu yake tarehe 15 Septemba, siku inayofuata sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba[1]. Hii ni kwa sababu, akisimama kwa uchungu chini yake na kumtolea Mungu sadaka hiyo, Maria alijitokeza kama Eva mpya: kama vile ukaidi wa mwanamke wa kwanza ulivyoleta kifo, utiifu wa ajabu wa huyo wa pili ulileta uzima kumpitia Mwanae mfufuka [2].
Ndivyo ilivyopangwa na Papa Pius X kwa dunia nzima mwaka 1913, baada ya heshima hiyo kuenea sana katika ya Wakatoliki kuanzia karne ya 11.
Msingi wake ni hasa habari za Injili ya Luka (2:34-35,41-51; 23:27-31,55-56) na ya Yohane (19:25-27), lakini pia ile ya Mathayo (2:13) kuhusu mtoto Yesu kudhulumiwa na mfalme Herode Mkuu.
Katika liturujia ya Neno, Misa ya siku hiyo ina sekwensya ya pekee, ambayo kwa Kilatini inaitwa "Stabat Mater" ("Mama alisimama"), ambayo ndiyo maneno ya kwanza ya shairi hilo lenye muziki wa huzuni lakini mtamu.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 329-331
- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 320-321
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 277-278
| Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Mateso kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |