Kurudi Nazareti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kurudi toka Misri kadiri ya James Tissot.
Familia takatifu kurudi toka Misri kadiri ya Jacob Jordaens (1616 hivi).
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Kurudi Nazareti kwa familia takatifu kutoka Misri ni tukio la utotoni mwa Yesu linalosimuliwa na Injili.

Mathayo na Luka sawia wanashuhudia kuwa Yesu alizaliwa Bethlehemu akakulia Nazareti[1][2].

Jambo linalosimuliwa na Injili ya Mathayo tu ni kwamba katikati Yosefu alielekezwa na malaika kukimbilia Misri na Bikira Maria na mtoto Yesu ili kukwepa maangamizi yaliyopangwa na Herode Mkuu dhidi ya watoto wachanga wa kiume wa Bethlehemu. Baada ya Herode kufariki[3][4][5], Yosefu alielekezwa tena kwenda kuishi Galilaya, si Yudea alipotawala Arkelao.[6][7]

Upande wake Injili ya Luka inasimulia tu kuwa Yosefu alikuwa anaishi Nazareth kabla ya Yesu kuzaliwa akarudi huko baada ya Yesu kutolewa hekaluni siku ya arubaini baada ya kuzaliwa.

Tukio hilo lilichorwa mara nyingi na wasanii[8]

Habari yenyewe katika Injili ya Mathayo[hariri | hariri chanzo]

2:1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,

6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,

Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda;

Kwa kuwa kwako atatoka mtawala

Atakayewachunga watu wangu Israeli.

7 Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. 8 Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie. 9 Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. 10 Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. 12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.

13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; 15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema,

Kutoka Misri nalimwita mwanangu.

16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi. 17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,

18 Sauti ilisikiwa Rama,

Kilio, na maombolezo mengi,

Raheli akiwalilia watoto wake,

Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.

19 Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. 21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. 22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, 23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Keener, Craig (2009). The Gospel of Matthew: A Socio-Rhetorical Commentary. Eerdmans. uk. 114. ISBN 9780802864987. Iliwekwa mnamo 28 November 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. IVP New Testament Commentaries, Growing Up in a Small Town, accessed 29 November 2016
  3. Schürer, Emil. A History of the Jewish People in the Time of Jesus Christ, 5 vols. New York, Scribner's, 1896.
  4. Barnes, Timothy David. "The Date of Herod's Death," Journal of Theological Studies ns 19 (1968), 204–219
  5. Bernegger, P. M. "Affirmation of Herod's Death in 4 B.C.", Journal of Theological Studies ns 34 (1983), 526–531.
  6. Bart D. Ehrman, Jesus: apocalyptic prophet of the new millennium, Oxford University Press 1999, page 38; Paula Fredriksen, From Jesus to Christ (Second edition, Yale University Press, 2000, page 36); R. T. France, The Gospel of Matthew (Wm. B. Eerdmans Publishing, 2007) page 43; Rudolf Schnackenburg, The Gospel of Matthew, (Wm. B. Eerdmans Publishing, 2002) page 27; Marcus Borg, 'The Meaning of the birth stories', in Borg and Wright, The Meaning of Jesus: Two Visions (HarperOne, 1999), page 180.
  7. "The Persecuted Child", Bible Gateway. 
  8. artistic representation
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kurudi Nazareti kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.