Nenda kwa yaliyomo

Galilaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moja ya sehemu za Galilaya

Galilaya (kutoka Kiebrania הגליל (ha-galil), yaani "mzunguko" au "mkoa"; kiasili "galil ha-goyim - mkoa wa wapagani") ni mkoa maarufu kihistoria upande wa kaskazini mwa Israeli au Palestina.

Upande wa mashariki mpaka wake ni mto Yordani, ambao sehemu hiyo unaunda ziwa Genesareti (pia: bahari ya Galilaya).

Waisraeli walipotoka Misri na kuteka nchi ya Kanaani, katika mkoa huo walihamia watu wa makabila ya Dan, Zebuluni, Isakari na Naftali.

Galilaya ndio mkoa ambapo alikulia na kuanza utume wake Yesu, mwanzilishi wa Ukristo.

Kati ya miji na vijiji vya Galilaya vilivyotajwa katika Injili kuna: