Nazareti
Jump to navigation
Jump to search
Nazareti (الناصرة kwa Kiarabu, נצרת kwa Kiebrania) ni mji wenye watu 65.000 upande wa kaskazini wa nchi ya Israeli, ambao kihistoria unajulikana kama Galilaya.
Wakazi wengi ni raia wa Israeli wanaoongea Kiarabu na kufuata dini za Uislamu (68,7%) na Ukristo (31,3%).
Nazareti unajulikana kama mji walipokulia Bikira Maria na mwanae Yesu Kristo, ambaye kadiri ya Injili, ingawa alizaliwa Bethlehemu, alikuwa anatajwa kama Mnazareti.