Bethlehemu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Betlehemu (kwa Kiarabu "بيت لحم") maana yake ni "Nyumba ya mkate" (kutoka Kiebrania, ambapo "לחם" = "Mkate") ni mji wa Palestina, maarufu hasa kama mahali alipozaliwa Yesu Kristo.

Kadiri ya Injili, ndivyo ulivyotimia utabiri wa kitabu cha Mika 5:1.

Mapokeo yanataja mahali hapo katika Basilika la Kuzaliwa.

Bethlehemu iko kilometa 10 hivi kusini kwa Yerusalemu, mita 765 juu ya usawa wa bahari.

Kadiri ya Biblia, Bethlehemu ndio mji asili wa Daudi, mfalme wa pili wa Israeli na babu wa Yesu katika mfululizo wa vizazi vingi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bethlehemu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.