Mama wa Mungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Theotokos)
Katika nakshi hii iliyopo kwenye Basilika la Hagia Sofia, huko Istanbul herufi za Kigiriki ΜΡ ΘΥ zinamaanisha Mama wa Mungu.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Mama wa Mungu (kwa Kigiriki Θεοτόκος, Theotókos; kwa Kilatini Deipara au Dei genetrix, yaani "Mzaa Mungu") ni sifa kuu ambayo Wakristo wengi wanampatia Bikira Maria mama wa Yesu Kristo.

Msingi wa imani hiyo[hariri | hariri chanzo]

Kwa kuwa wafuasi wa Yesu wanasadiki kuwa yeye ni Mungu sawa na Baba, wengi wao wanakubali kuwa aliyemzaa kama binadamu anastahili kuitwa Mama wa Mungu.

Dogma[hariri | hariri chanzo]

Sifa hiyo ilianza kutumika katika karne ya 2, labda nchini Misri, ikathibitishwa moja kwa moja na Mtaguso wa Efeso (431) dhidi ya Patriarki Nestori aliyedai anaweza kuitwa tu Mama wa Yesu au Mama wa Kristo.

Mtaguso mkuu huo uliona kwamba Nestori alimgawa Yesu katika nafsi mbili: ya Kimungu na ya kibinadamu. Kumbe imani sahihi inamkiri kwamba nafsi ya Yesu ni ile ya Kimungu tu ambayo ni ya pili katika Utatu Mtakatifu. Hivyo aliyemzaa Yesu kama binadamu (si kama Mungu, jambo ambalo haliwezekani) anastahili kuitwa Mama wa Mungu (upande wa ubinadamu wake alioutwaa kwake).

Heshima katika sala[hariri | hariri chanzo]

Kwa namna ya pekee, Maria anapewa sifa hiyo katika sala ya Salamu Maria, iliyo maarufu zaidi kati ya sala za Ukristo wa magharibi kwa mama wa Yesu.

Adhimisho katika liturujia[hariri | hariri chanzo]

Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki wanaofuata mapokeo ya Kanisa la Roma tarehe 1 Januari, siku ya nane (Oktava) ya Noeli, lakini Wakatoliki wengine wanaiadhimisha siku tofauti, kwa mfano huko Milano ni Jumapili kabla ya Noeli.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mama wa Mungu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.