Maria kupalizwa mbinguni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mchoro wa Tiziano, katika Basilika la Santa Maria Gloriosa dei Frari, Venezia, Italia. Labda mchoro huo wa mwaka 1516-1518 ni maarufu kuliko yote ya Kanisa la Magharibi kuhusu fumbo hilo.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
StPetersBasilicaEarlyMorning.jpg
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Maria kupalizwa mbinguni ni sherehe ya Kanisa Katoliki inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Agosti. Kadiri ya sheria za Kanisa, kimataifa ni sikukuu ya amri, ingawa katika nchi nyingine si hivyo, kutokana na serikali kutokubali tarehe hiyo kama siku ya pumziko.

Msingi katika imani[hariri | hariri chanzo]

Adhimisho hilo la liturujia ni la zamani, lakini limepata nguvu mpya kutokana na dogma iliyotangazwa na Papa Pius XII kwa hati Munificentissimus Deus ya tarehe 1 Novemba 1950 baada ya kusikiliza maoni ya maaskofu wote duniani.

Fundisho hilo la imani Katoliki ni kwamba Bikira Maria, mama wa Yesu, alipomaliza maisha yake duniani alichukuliwa mwili na roho mbinguni, ashiriki mapema utukufu wa Mwanae mfufuka, Yesu Kristo kama alivyoshirikiana naye toka mwanzo hadi mwisho wa maisha yake.

Fundisho hilo linalingana na lile la Waorthodoksi, ingawa hao hawajalitangaza kuwa dogma. Tarehe hiyohiyo wao wanaadhimisha ya Kulala kwa Bikira Maria.

Hata baadhi ya Waanglikana na Walutheri wana adhimisho la Bikira Maria siku hiyo.

Umoja wa msimamo huo upande wa mashariki na wa magharibi wa Kanisa unatokana na mapokeo ya karne za kwanza za Ukristo, yanayoshuhudiwa na mababu wa Kanisa kama vile Efrem wa Syria, Timoteo wa Yerusalemu, Epifanio wa Salamina na Yohane wa Damasko.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria kupalizwa mbinguni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.