Kanisa la Magharibi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Matawi ya Ukristo yalivyotokea katika historia ya Kanisa. Upande wa juu ndio Kanisa la Magharibi, upande wa chini Makanisa ya Mashariki. Unene wa mistari haulingani na ukubwa wa madhehebu husika.

Kanisa la Magharibi (au Ukristo wa Magharibi) linajumlisha Kanisa la Kilatini na madhehebu mengine yaliyotokea upande wa magharibi wa Bahari ya Kati yakiwa na mwelekeo tofauti na ile ya Makanisa ya Mashariki.

Katika Karne za kati, taratibu Kanisa la Roma liliunganisha magharibi yote chini yake, hata kwa kufuta mapokeo tofauti, kama ya Makanisa ya Kiselti katika visiwa vya Britania.

Hata baada ya Kanisa la Magharibi kupatwa na mafarakano mengi hasa katika karne ya 16, bado kuna mambo mengi yanayofananisha Kanisa la Kilatini na madhehebu mengi ya Uprotestanti.

Ndiyo aina ya Ukristo iliyoenea zaidi duniani (80% hivi) pamoja na ustaarabu wa magharibi ulioathiriwa nayo.