Teolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Teolojia, pia theolojia[1] (Kigiriki θέος theos "Mungu" + λογία logia "usemi") ni elimu juu ya Mungu hasa katika Ukristo. Hiyo haitenganiki na utendaji wake wa nje, yaani uhusiano wake na viumbe vyote.

[2]

Kumbe ikitajwa kwa jina la mkopo kutoka Kigiriki, fani hiyo inachunguza hasa imani ya Kikristo kadiri ya Ufunuo wa Mungu uliokamilika katika Yesu Kristo na Mitume wake.

Kwa sababu hiyo inategemea hasa Maandiko Matakatifu ya Biblia, lakini pia, kadiri ya madhehebu husika, Mapokeo ya Mitume yasiyoandikwa na mamlaka hai ya Kanisa (Ualimu).

Teolojia hufundishwa katika vyuo na katika nchi mbalimbali iko pia kama idara ya Chuo Kikuu. Idara hizi mara nyingi zinatenganishwa kidhehebu. Mtu aliyepita mafundisho ya chuo huitwa mwanateolojia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tahajia ya "teolojia" ni kawaida katika kanisa katoliki, "theolojia" zaidi kati ya WaprotestantiMaandishi ya italiki
  2. Jina lingine la fani hiyo lenye asili ya Kiarabu ni Tauhidi. Hilo linatumiwa zaidi na Waislamu.