Mwanatheolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mwanateolojia)

Mwanatheolojia ni mtu anayeshughulikia theolojia au ujuzi juu ya habari za Mungu kitaalamu. Ni tofauti na mtaalamu wa dini anayeweza kuchungulia dini yoyote, kwa sababu mwanatheolojia ana msimamo katika mapokeo ya dini moja hasa.

Si lazima awe mwalimu wa dini yake anayetambuliwa na waumini, kwa sababu kitambulisho ni kiwango chake cha elimu si imani. Hata hivyo kuna pia wanatheolojia ambao mara nyingi ni viongozi wa kiroho.

Katika mapokeo ya Ukristo wa magharibi mwanatheolojia amepita ngazi za chuo kikuu na masomo yake katika idara ya theolojia. Nje ya Ukristo wa magharibi kwa mfano katika Uislamu, Uyahudi na Ukristo wa mashariki kuna pia njia mbalimbali za kukubaliwa kufika kwenye kiwango cha utaalamu wa habari za Mungu.

Katika muundo wa theolojia ya magharibi mwanatheolojia ataweka mkazo wake katika masomo ya theolojia kama vile:

na mengineyo.