Mchungaji
Mchungaji ni mtu anayechunga mifugo, kama vile kondoo, lakini pia watu, hasa katika Ukristo, ambapo ni cheo maalumu katika madhehebu ya Uprotestanti.
Kihistoria, uchungaji ulianza katika Mashariki ya Kati miaka 5,000 hivi iliyopita.
Katika Biblia kazi hiyo ilitumika sana kufafanua majukumu ya wafalme na viongozi wengine. Daudi alichukuliwa kama kielelezo.
Manabii walitabiri ujio wa mwana wa Daudi atakayechunga vizuri taifa la Israeli kwa niaba ya Mungu.
Yesu alijitambulisha kama mchungaji mwema aliye tayari kutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake (Yoh 10:11).
Mwenyewe alimkabidhi Mtume Petro uchungaji wa kundi lake (Yoh 21:16).
Mfano huo unatumika pia kwa watu wengine (Mdo 20:17,28; 1Kor 9:7; Ef 4:11; 1Pet 5:12).
Katika ibada Maaskofu wa Kanisa Katoliki na wengineo wanatumia bakora kujitambulisha kama wachungaji.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Bercot, David W. (1999). Will The Real Heretics Please Stand Up. Scroll Publishing. ISBN 0-924722-00-2.
- Dowly, Tim (ed.) (1977). The History of Christianity. Lion Publishing. ISBN 0-7459-1625-2.
{{cite book}}
:|author=
has generic name (help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Maana ya kawaida
[hariri | hariri chanzo]- A Beginner's Guide to Raising Sheep
- A Shepherds Songbook
- American Karakul Sheep Registry
- American Livestock Breeds Conservancy
- Rare Breeds Conservation Society of New Zealand
- Scottish Blackface Sheep Breeders Association
Maana ya kidini
[hariri | hariri chanzo]- NewAdvent.org, The Catholic Encyclopedia's entry on the term pastor.
- LifeWay.com Ilihifadhiwa 14 Juni 2011 kwenye Wayback Machine., Articles to help the pastor in the roles of preacher, missionary, leader, shepherd, and person.
- Nacministers.com Ilihifadhiwa 3 Desemba 2018 kwenye Wayback Machine., Priesthood of All Believers: Explained and Supported in Scripture
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mchungaji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |