Nenda kwa yaliyomo

Mifugo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchungaji na mifugo yake
Mifugo aina ya ng'ombe
Ng'ombe machungani.
Ng'ombe aina ya Żubroń.
Mifugo ya nyumbani

Mifugo (kutoka kitenzi "kufuga"; pia: Wanyama wa kufugwa au wanyama-kaya) ni wanyama wanaopatikana kutokana na ufugaji wa kibinadamu.

Wako tofauti na wanyamapori baada ya na mchakato mrefu ambako wanyama wa pori ama walijiunga na binadamu au walishikwa nao na watoto wao kuteuliwa kutokana na tabia zilizopendelewa na wafugaji wao. Tabia hizo ni pamoja na upole na uwezo wa kupatana na binadamu, uwezo wa kuzalisha kiasi fulani cha nyama au maziwa, uwezo wa kustawi kwa chakula fulani au katika mazingira mbalimbali.

Katika mchakato wa vizazi vingi tabia zilizolengwa ziliimarishwa katika spishi zinazofugwa.

Uteuzi huu umesababisha tofauti za kimaumbile na tofauti za tabia baina ya wanyama wa kufugwa na wanyamapori wa spishi ileile. Tofauti hizi zinaonekana katika rangi, ukubwa wa mwili, uwezo wa kuwasiliana na binadamu na mengine.

Asili katika wanyama waliotafuta mazingira ya kibinadamu

[hariri | hariri chanzo]

Imethibitishwa ya kwamba mnyama wa kwanza wa kufugwa alikuwa mbwa. Asili ya mbwa walikuwa vikundi vya mbwa mwitu wa Ulaya (wolf) waliofuata koo za binadamu wawindaji na kula mabaki ya chakula yaliyotupwa nao. Kwa kupatana na mbwa mwitu ambao walikuwa wapole na kutoshambulia watu (pamoja na kuua wote waliokuwa wakali) binadamu hao walianza kupatana nao na kuona faida ya uangalifu wao wakati mgeni au windo alikaribia. Tangu kuwapatia mbwa mwitu chakula kama zawadi waliendelea kuzoeana. Ingawa historia hii bado haieleweki kikamilifu, watalaamu wengine wanaona ya kwamba wawindaji kadhaa walianza kutunza watoto wa mbwa mwitu kwao na kuwafuga kama wanyama wapenzi.

Inaonekana ya kwamba kulikuwa pia na wanyama wengine wa porini waliofuata binadamu kwa sababu waliona faida kukaa karibu nao kama vile paka (aliyefuata panya waliokula mavuno ya wakulima wa kwanza).

Vilevile asili ya kuku ni kuku mwekundu wa porini wa Indonesia (red junglefowl) aliyetafuta takataka kwenye makazi ya watu, akawazoea na kutumiwa nao kama chanzo cha nyama na mayai.

Wanyama wa nyumbani ni wale ambao huishi katika mazingira ambayo mwanadamu anaishi na hawawezi kumuathiri kwa kiasi kikubwa. Wanyama hao wanatunzwa kwa uangalizi wa binadamu kwa ajili ya ulinzi, michezo, kazi, pambo na majaribio ya maabara.

Tangu milenia kadhaa wanyama hao wamepatana na wanadamu, nao ni kama vile mbwa, mbuzi, nguruwe, kondoo, ng'ombe, paka, kuku, punda, bata, nyuki, ngamia, farasi, njiwa, kware na wengine wengi.

Wanyama hao wana faida katika maisha ya wanadamu; kwa mfano:

  • ng'ombe hupatia watu maziwa, nyama, pia ngozi yake inaweza kutumika kutengeneea vitu mbalimbali.
  • mbwa husaidia hasa katika suala la ulinzi katika mazingira yanayomzunguka mwanadamu.
  • mbuzi huwapatia watu nyama, maziwa ila si mazuri kama yale ya ng'ombe na pia ngozi yake hutumika kutengenezea vitu kama vile ngoma, hasa katika jamii za Afrika.
  • kware ni ndege mdogo; mayai yake ni madogo sana yana faida kubwa katika mwili wa mwanadamu kwa sababu yanasemekena kutibu baadhi ya magonjwa katika miili yetu.

Mifugo hii huwa na faida nyingi sana kwa mwanadamu, kwa hiyo anashauriwa kuwafuga kwa ajili ya faida zifuatazo:

  • 1. Mifugo kama vile ng'ombe na mbuzi hutupatia maziwa ambayo hutusaidia kupata protini ambayo husaidia mwili kukua na pia huulinda mwili dhidi ya magonjwa.
  • 2. Mifugo pia hutupatia nyama, ambayo hutupata protini ambayo husaidia mwili kukua na pia kulinda mwili dhidi ya magonjwa.
  • 3. Mifugo hutupatia pesa kwa kuuza nyama, maziwa, ngozi, kwato, mbolea na hata wanyama wenyewe.
  • 4. Ngozi ya mifugo hutumika kutengenezea vitu kama vile ngoma, viatu, mikanda, nguo. Vitu vinavyotengenezwa kwa kutumia ngozi ni imara na pia hudumu kwa muda mrefu.
  • 5. Kwato za wanyama hawa hutumika kutengenezea vyombo kama sahani,vibakuli, na kadhalika.
  • 6. Mavi ya wanyama hutumika kama mbolea ambayo huwezesha mazao kukua haraka na kustawi vizuri.
  • 7. Wanyama pia hutumika kwa tiba. Wagonjwa wanaohitaji wanyama katika matibabu yao hupewa ruhusa maalum kusafiri na kuishi na wanyama hata sehemu ambazo wanyama hawakubaliwi.

Wanyama wana faida nyingi sana; hizi ni chache tu. Wanyama hao hutoa pia faida za kihisia kama mazoezi, mahusiano ya kijamii na n.k. Wanyama hawa huondoa upweke kwa watu wasiokuwa na marafiki au mahusiano ya kijamii kama wazee, watoto, wajawazito. Wanyama wengine huwatembelea wagonjwa.

Wanyama hawa hufundihswa jinsi ya kufanya vitu vya kisayansi, kwa kulenga wagonjwa.

Hivyo tunaweza kuona faida za wanyama hao: inafaa tuwatunze vizuri kwani tunawategemea katika shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi. Hivyo hawatakiwi kupigwa ovyo. Wanatakiwa waangaliwe afya zao na kupata mahitaji yao.

  • [www.palaeobarn.com/sites/domestication.org.uk/files/downloads/112.pdf Larson, Fuller:The Evolution of Animal Domestication]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mifugo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.