Mbwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mbwa
Mbwa-mwitu wa Ulaya
Mbwa-mwitu wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa)
Jenasi: Atelocynus Cabrera, 1940

Canis Linnaeus, 1758
Cerdocyon C.E.H. Smith, 1839
Chrysocyon C.E.H. Smith, 1839
Cuon Hodgson, 1838
Lycalopex Burmeister, 1854
Lycaon Brookes, 1827
Nyctereutes Temminck, 1839
Otocyon Müller, 1836
Speothos Lund, 1839
Urocyon Baird, 1857
Vulpes Frisch, 1775

Mbwa ni wanyama mbua wa familia Canidae, lakini takriban spishi zote za Afrika zinaitwa bweha au mbweha.

Ukubwa wa spishi za mwitu unatofautiana kutoka 24 sm (fenek) mpaka 2 m (mbwa-mwitu wa Ulaya (kadiri ya vipimo kwa mbwa-kaya ni 9.5-250 sm).

Wanyama hawa wana pua ndefu na miguu mirefu na mkia wa manywele. Rangi yao ni kijivu, kahawia au hudhurungi; kwa kawaida tumbo ni jeupe.

Spishi nyingine zinatokea misitu na nyingine zinatokea maeneo wazi. Mbwa hukamata mawindo aina yo yote lakini ukubwa wa mawindo unafuatana na ukubwa wa spishi ya mbwa. Hata hivyo, spishi zinazoishi kwa makundi, kama mbwa-mwitu wa Afrika, zinaweza kukamata windo kubwa sana kuliko wao wenyewe. Spishi kadhaa hufugwa, hususan mbwa-kaya.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]