Bweha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bweha
Bweha mgongo-mweusi (Canis mesomelas)
Bweha mgongo-mweusi (Canis mesomelas)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mammalia Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha watoto wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa)
Fischer, 1817
Jenasi: Canis Linnaeus, 1758

Cerdocyon C.E.H. Smith, 1839
Lycalopex Burmeister, 1854
Otocyon Müller, 1836
Urocyon Baird, 1857
Vulpes A. Frisch, 1775

Bweha au mbweha ni mojawapo wa wanyama wadogo kiasi wa familia Canidae wanaopatikana Afrika, Amerika, Asia na Ulaya na walioainishwa katika jenasi Canis, Cerdocyon, Lycalopex, Otocyon, Urocyon na Vulpes.

Spishi za bweha katika jenasi Canis zina mnasaba sana na mbwa-mwitu. Kwa ukweli, siku hizi Canis anthus na Canis aureus zinafikiriwa kuwa mbwa-mwitu[1][2], lakini kwa sasa jina "bweha" litadumishwa kwa sababu linatumika sana.

Usasi (Uwindaji) wa bweha[hariri | hariri chanzo]

Kwa muda mrefu, usasi wa bweha umeonekana kwamba umejikita mizizi tu kwa wazungu ambako wao huchukua mbwa na farasi na kwenda huku wakiwawinda bweha. Hili limebadilika huku hata Waafrika wakiwawinda bweha.

Mbwa wawinda-bweha huweza kutumia hisia na kuwawinda bweha wekundu. Tendo hili la kuwawinda bweha limezua hisia tofauti huku wengi wakiliona kana kwamba lamfanya bweha awe matatani kulingana na hariri la Wild Hunter Club.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Koepfli, K.-P.; Pollinger, J.; Godinho, R.; Robinson, J.; Lea, A.; Hendricks, S.; Schweizer, R. M.; Thalmann, O. et al. (2015-08-17). "Genome-wide Evidence Reveals that African and Eurasian Golden Jackals Are Distinct Species". Current Biology 25: 2158–65. doi:10.1016/j.cub.2015.06.060 . PMID 26234211 . http://www.cell.com/current-biology/abstract/S0960-9822%2815%2900787-3.
  2. (Kihispania) Urios, Vicente; Donat-Torres, Maria P.; Ramírez, Carlos; Monroy-Vilchis, Octavio; Hamid Rgribi-Idrissi (2015): El análisis del genoma mitocondrial del cánido estudiado en Marruecos manifiesta que no es ni lobo (Canis lupus) ni chacal euroasiático (Canis aureus). figshare. doi:10.6084/m9.figshare.1524971