Bweha Dhahabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bweha dhahabu
Golden wolf small.jpg
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa)
Nusufamilia: Caninae
Jenasi: Canis
Linnaeus, 1758
Spishi: C. aureus
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Nususpishi 13:
C. a. algirensis
C. a. anthus
C. a. aureus
C. a. bea
C. a. cruesemanni
C. a. ecsedensis
C. a. indicus
C. a. lupaster
C. a. moreotica
C. a. naria
C. a. riparius
C. a. soudanicus
C. a. syriacus

Bweha dhahabu (pia bweha-dhahabu, mbweha dhahabu) ni mnyama wa jamii ya mbwa na mwenyeji wa Afrika ya Kaskazini na Mashariki na Mashariki ya Kati, akaenea pia hadi Ulaya ya Kusini.

Anapatikana pote Tanzania ambayo ni kusini kabisa ya uenezaji wake hadi sasa. Hata akiitwa bweha yuko karibu zaidi na Mbwa-mwitu Habeshi na coyote (mbwa-nyika) wa Amerika ya Kaskazini.

Anakula wanyama wadogo, mizoga, wadudu na matunda. Makazi yake kwenye mbuga na misitu myepesi. Anaishi kwa vikundi vidogo hasa dume na jike pamoja na watoto.

Kwa jumla kuna nususpishi 13 zinazotambuliwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Sillero-Zubiri, C. (2009). Family Canidae (Dogs). (352-447). In: Wilson, D. E., Mittermeier, R. A., (Hrsg.). Handbook of the Mammals of the World. Volume 1: Carnivores. Lynx Edicions, 2009. ISBN 978-84-96553-49-1