Mbwa-mwitu Dhahabu
Mbwa-mwitu dhahabu | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bweha mashariki (Canis anthus bea)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nususpishi 6:
| ||||||||||||||||||
Msambao wa mbwa-mwitu dhahabu
|
Mbwa-mwitu dhahabu (pia bweha-dhahabu, bwea dhahabu, mbweha dhahabu na bweha-mbuga) ni mnyama wa jamii ya mbwa anayetokea Afrika ya Kaskazini na ya Mashariki. Zamani jina lake la kisayansi lilikuwa Canis aureus, lakini hivi karibuni wataalamu wamebaini kwamba nususpishi za Afrika ni tofauti na zile za Asia na Ulaya. Kwa hivyo nususpishi za Afrika zimepata jina jipya Canis anthus[1]. Hadi sasa bado huitwa bweha na watu wengi lakini yuko karibu zaidi na Mbwa-mwitu Habeshi na Mbwa-nyika (coyote) wa Amerika ya Kaskazini. Kwa hivyo tafadhali aitwe mbwa-mwitu.
Anapatikana Kenya na kaskazini kwa Tanzania (k.m. Hifadhi ya Serengeti) ambayo ni kusini kabisa ya uenezaji wake.
Mbwa-mwitu dhahabu hula wanyama wadogo hadi ukubwa wa swala, mizoga, wadudu na matunda. Makazi yake ni jangwa, mbuga na misitu myepesi. Anaishi kwa vikundi vidogo hasa dume na jike pamoja na watoto.
Kwa jumla kuna nususpishi 6 zinazo tambuliwa:
- Canis a. algirensis, Mbwa-mwitu wa Aljeria au Bweha Kaskazi (Algerian wolf)
- Canis a. anthus, Mbwa-mwitu au Bweha wa Senegali (Senegalese wolf)
- Canis a. bea, Mbwa-mwitu au Bweha Mashariki (Serengeti wolf)
- Canis a. lupaster, Mbwa-mwitu au Bweha wa Misri (Egyptian wolf)
- Canis a. riparius, Mbwa-mwitu au Bweha Somali (Somali wolf)
- Canis a. soudanicus, Mbwa-mwitu Mabaka au Bweha wa Sudani (Variegated wolf)
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Koepfli, K.-P.; Pollinger, J.; Godinho, R.; Robinson, J.; Lea, A.; Hendricks, S.; Schweizer, R. M.; Thalmann, O.; Silva, P.; Fan, Z.; Yurchenko, A. A.; Dobrynin, P.; Makunin, A.; Cahill, J. A.; Shapiro, B.; Álvares, F.; Brito, J. C.; Geffen, E.; Leonard, J. A.; Helgen, K. M.; Johnson, W. E.; O'Brien, S. J.; Van Valkenburgh, B.; Wayne, R. K. (2015-08-17). "Genome-wide Evidence Reveals that African and Eurasian Golden Jackals Are Distinct Species". Current Biology. 25: 2158–65. doi:10.1016/j.cub.2015.06.060. PMID 26234211.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Sillero-Zubiri, C. (2009). Family Canidae (Dogs). (352-447). In: Wilson, D. E., Mittermeier, R. A., (Hrsg.). Handbook of the Mammals of the World. Volume 1: Carnivores. Lynx Edicions, 2009. ISBN 978-84-96553-49-1