Mbwa-kaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mbwa
Coat types 3.jpg
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa)
Jenasi: Canis (Mbwa)
Linnaeus, 1758
Spishi: C. lupus
Linnaeus, 1758
Nususpishi: C. l. familiaris
(Linnaeus]], 1758)

Mbwa (Canis lupus familiaris) ni mnyama anayefugwa na binadamu tangu muda mrefu. Kibiolojia anahesabiwa kati ya mamalia wanaokula nyama.

Tangulizi[hariri | hariri chanzo]

Mbwa, kisayansi Canis lupus familiaris, ni jamii ya mbwa mwitu wanaohusishwa na binadamu. Mbwa kwa muda mrefu, wamekuwa pamoja na binadamu, wakisaidia kazi mbalimbali na kuwa kampani ya binadamu. Mbwa, walikuwa na thamani kubwa sana kwa binadamu wa kale walisaidia ulinzi, uwindaji, kuchunga mifugo, kusaidia polisi na wanajeshi, na sasa mpaka kuwasaidia watu wenye ulemavu. Tabia hizi zinawafanya kuonekana ndio wanyama rafiki wa binadamu kuliko wengine wote. Mpaka sasa inakadiriwa kuwa kuna mbwa milioni 400 duniani kote.

Watu na mbwa[hariri | hariri chanzo]

Watu wametumia mbwa kulingana na utamaduni wao kwa njia mbalimbali kama mnyama wa kazi akilinda nyumba na mifugo au kubeba mzigo.

 • Waeskimo wa Aktiki wanatumia mbwa kwa usafiri wakivuta sleji yaani vitoroli vinavyoteleza juu ya barafu.
 • Watu wa China Kusini, Korea na Vietnam wanakula nyama ya mbwa. Inakadiriwa kuwa mbwa kati ya milioni 13-16 huliwa kila mwaka katika bara la Asia.
 • Mara nyingi mbwa wanafugwa nyumbani kama wanyama wa kusindikiza watu tu wakitazamiwa kama marafiki.
 • Kinyume chake katika utamaduni mwingine mbwa anaangaliwa kama najisi.

Mbwa wametumiwa kwa kazi nyingi.

 • Wanalinda nyumba za watu.
 • Wanaangalia na kulinda mifugo kwa mfano kondoo
 • Wanaongoza watu vipofu,
 • wanasaidi polisi,
 • wanatafuta madawa ya kulevya au mabomu yaliyofichwa.
 • Kiumbe cha kwanza kilichotoka duniani alikuwa mbwa jike Laika aliyerushwa angani tar. 3 Novemba 1957 kwa chombo cha angani cha kirusi Sputnik 2 akafa huko siku ileile.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na historia ndefu ya kufugwa na uteuzi wa kibinadamu kuna aina nyingi za mbwa wanaoonyesha miili tofautitofauti, Hata hivyo mbwa wote ni spishi moja tu na wote wanaweza kuzaa pamoja.

Mbwa huwa na uwezo mzuri wa kusikia na kunusa lakini hawaoni vizuri sana hasa rangi. Wanaweza kusikia sauti kwa umbali wa kilomita kadhaa.

Mbwa wengi hufikia umri wa kati ya miaka 10 na 13.[1]


Kiasili mbwa waliishi katika makundi yenye ufuatano wa vyeo. Mbwa mkuu huitwa "dume alfa". Mbwa wakiishi pamoja na binadamu wanawakubali kama mbwa wenye cheo cha juu.

Utafiti unaonyesha kuwa kutokana na kuishi na binadamu wa muda mrefu, mbwa wana uelewa wa pekee wa tabia za binadamu.[2] Mbwa kaya wanaweza kuishi kwa kula chakula cha wanga tu wakati aina nyingine za mbwa haziwezi.

Biolojia[hariri | hariri chanzo]

Mbwa wamekuwa wakikuzwa kwa makusudi mbali duniani, kutokana na uwezo wao wa hisia na kutumia maungo yao. Mbwa hutofautiana sana kwa vizazi vyao hasa katika muonekano, ukubwa na tabia kuliko wanyama wengine wowote. Hata hivyo maungo yao yanasimama kwa ajili yao, mbwa mwitu wa kafiawia. Mbwa hula nyama kwa kuwinda, na mabaki, na kama ilivyo kwa wanyama wengi wala nyama (wawindaji), mbwa wana misuli yenye nguvu, mifupa inayomruhusu kuruka na uvumilivu pamoja na meno kwa ajili ya kukamata na kurarua. Mbwa hutofautiana sana kwa ukubwa na uzito.

Uoni[hariri | hariri chanzo]

Kama ilivyo kwa wanyama wengi, mbwa huwa hawaoni kwa rangi zote kama binadamu, na badala yake kwa bluu na nyekundu tu . Uoni wa mbwa umeimarika kutokana na shughuli zake za uwindaji. Hata hivyo mbwa wameonekana mahiri zaidi katika utambuzi wa vitu vilivyo katika mwendo, hasa pale wanapowatambua wamiliki wao, hata wakiwa kilometa moja kutoka kwa mbwa.

Kusikia[hariri | hariri chanzo]

Uwezo wa kusikia wa mbwa ni zaidi ya ule wa binadamu, hivyo mbwa huweza kusikia hata sauti ndogo kabisa ambazo binadamu hawezi kuzisikia. Wana uwezo mkubwa sana wa kujua hata sehemu ilipotokea sauti Wana misuli kumi na nane inayoweza kugeuza, kuinua, kushusha na kuzungusha masikio.

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na kuwa na asili ya mbwa mwitu ambao ni wala nyama, chakula cha mbwa ni cha aina mbalimbali na sio nyama pekee. Licha ya nyama mbwa hula mboga na nafaka. Kiafya haishauriwi kuwapa mbwa chakula cha nyama peke yake kutokana na ukosefu wa madini ya chuma na kalsiamu. Ukilinganisha na mbwa mwitu, mbwa-kaya wana uwezo mkubwa wa kula vyakula vya wanga.

Dini na Tamaduni[hariri | hariri chanzo]

Katika dini ya Uislamu, mbwa huonekana kama najisi. Kwenye dini na utamaduni wa Kiyahudi mbwa hutunzwa kama wanyama wengine wanaoishi na binadamu. Sheria ya Kiyahudi inahitaji Wayahudi kulisha mbwa (na wanyama wengine) kabla yao wenyewe, na kupanga jinsi ya kuwalisha kabla ya kuanza kuishi nao. Katika Ukristo, mbwa huonekana kama ni alama ya uaminifu.

Huko Uchina, Korea, na Japani, mbwa huchukuliwa kuwa ni walinzi.

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Filamu mbalimbali zimetolewa zinazohusu mbwa. Mojawapo ni The Fox and the Hound (KiswahiliMbweha na Mbwa), filamu ya katuni iliyotolewa mwaka wa 1981.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 1. Dog Longevity Web Site, Breed Data page.
 2. Functional MRI in Awake Unrestrained Dogs.