Nenda kwa yaliyomo

Kibonzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Katuni)

Kibonzo, pia Katuni (kutoka Kiingereza cartoons) au Komiki (kutoka Kiing. comics) ni namna ya kueleza hadithi au habari kwa kutumia picha. Picha hizi mara nyingi zimechorwa ama moja-moja au mfululizo na kueleza habari kwa namna ya kuchekesha.

Majadiliano ya wahusika kwenye kibonzo huonyeshwa kwa njia za viputo vya maneno. Kuna pia viputo vya dhana vya kuonyesha fikra za wahusika.

Kibonzo huonyeshwa mara nyingi kwenye magazeti. Kuna pia vitabu vya vibonzo vilivyokusanywa au vilivyochorwa moja kwa moja kama kitabu.

Kati ya vibonzo vinavyojulikana sana kimataifa kuna vile vya Walt Disney aliyeunda Mickey Mouse na wenzake.

Siku za nyuma vibonzo vya manga kutoka Japani vimepata wasomaji wengi kati ya vijana.

Kati ya wachoraji wa vibonzo wanaojulikana katika Afrika ya Mashariki kuna Godfrey Mwampembwa anayejulikana zaidi kwa jina "Gado" akionyesha kazi zake katika Daily Nation ya Nairobi.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]