Kuku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kuku
Kuku: Jogoo na tembe
Kuku: Jogoo na tembe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Galliformes (Ndege kama kuku)
Familia: Phasianidae (Ndege walio mnasaba na kwale)
Jenasi: Gallus
Brisson, 1760
Spishi: Gallus gallus (Kuku)
Linnaeus, 1758
Nususpishi: Gallus gallus domesticus

Kuku ni ndege anayefugwa na binadamu tangu miaka 8,000 hivi. Watu hutumia nyama yake na mayai kama chakula. Katika nchi ya baridi malaika yao ambayo ni manyoya madogo ya chini yanatumiwa kwa kujaza mashuka au makoti. Samadi ya kuku ni mbolea mzuri lakini inapaswa kukaa kwa muda kabla ya kutumiwa.

Kuku dume huitwa jogoo na jike ni tembe; mtoto wa kuku ni kifaranga. Kutokana na ufugaji uwezo wa kuruka umepotea.

Idadi ya kuku duniani inakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 10 na wengi wanafugwa kwa wingi wakiotamiwa na kuishi zizini. Kwa njia ya ufugaji aina nyingi za kuku zimeendelezwa kwa kuchagua wanyama wenye tabia maalumu na kuzaliana. Wanaofugwa siku hizi ni aina zinazotoa hasa nyama na aina nyingine zinatoa hasa mayai.

Katika mazingira asilia kuku huishi miaka 5-11 lakini wale wanaofugwa kwa wingi wanachinjwa baada ya wiki 6-8 kama ni kuku wa nyama na mwaka mmoja kama ni kuku wa mayai. Kati ya aina zinazofugwa kwa mayai karibu madume wote, yaani nusu ya vifaranga, wanauawa mara moja kwa sababu hawatagi mayai na aina hii haileti nyama ya kutosha.

Asili ya kuku zetu ni kuku mwitu wa [Indonesia]]. Ufugaji wake ulisambazwa Asia Bara na Polynesia. Mabaki ya mifupa ya kuku yamepatikana China yakiwa na umri wa miaka 8,000. Kutoka Asia ya Kusini-Magharibi kuku walisambazwa Uhindi na kupita Uajemi hadi Ugiriki na sehemu nyingine za Ulaya. Inaaminiwa ya kwamba kuku waliletwa Amerika Kusini kabla ya kuja kwa Kolumbus kupitia Pasifiki.

Utangulizi[hariri | hariri chanzo]

Kuku, kisayansi Gallus galena – domestians’, ni ndege anayefugwa nyumbani akiwa ni miongoni mwa wanyama waliosambaa zaidi duniani. Mpaka kufikia bilioni 24 mwaka 2003, kuku ndio ndege walio wengi zaidi duniani. Binadamu huwatunza kuku majumbani mwao kama chanzo cha chakula, hasa ikiwa nyama na mayai yao.

Ilisemekana kuwa, kuku walianza huko India, lakini ushahidi wa sasa unaonyesha kuwa walianza huko Vietnam miaka 10,000 iliyopita, kisha wakaenea mapaka Ugiriki, Misri n.k.

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Kuku hula majani na nyama. Wakiwa mwituni mara nyingi huonekana wakitumia muda wao mwingi kuparua-parua kutafuta mbegu, wadudu na hata wanyama wakubwa kama vile mijusi na panya pori wadogo.

Kuku huweza kuishi kwa miaka mitano mpaka kumi na moja kadiri ya spishi husika. Kuku wa biashara hukua kwa wiki sita tu kabla ya kuchinjwa. Kuku wanaokula kwa kutangatanga huweza kuchinjwa kuanzia wiki ya 14 na kuendelea. Kuku maalumu wa mayai huweza hata kutaga mayai 300 kwa mwaka kila mmoja. Baada ya mwaka mmoja uwezo wa kuku kutaga hupungua na kuku hao huchinjwa kwa ajili ya nyama. Kuku aliyevunja rekodi ya dunia, ni yule aliyeishi kwa zaidi ya miaka 16.

Baiolojia ya kawaida ya mazingira, kuku dume, jogoo, hutofautiana na kuku jike, tena kwa mwonekano wao. Majogoo huwa na kilemba na mkia maridadi, huku wakiwa pia na manyoya marefu mgongoni na shingoni mwao. Japo kuna baadhi ya aina ya kuku, ambao jogoo hawana kilemba chao, isipokuwa tu manyoya mengi.

Kuku wafugwao hawana uwezo mkubwa wa kuruka, japokuwa kuku wepesi wana uwezo wa kuruka juu ya uzio, kuta. Mara kadhaa kuku huruka kuyatizama mazingira yao, lakini mara nyingi huwa juu ya kuwakimbia adui.

Kuku huwa na tabia ya kutaga mayai kwenye kiota ambacho kina mayai tayari. Baadhi ya wakulima hutumia mayai ya unsushi ili kuwavutia kuku watage maeneo wanayoyataka wao.

Kuku pia huwa wasumbufu sana kuhusu mahali panapowafaa kutumika kwa majogoo huashiria uwepo katika himaya yake kwa majogoo wengine. Hata hivyo mara nyingine kuwika huwa ni kutokana na kusumbulia mara kadhaa. Temba hutumika mara baada ya kutaga na pia wakati wa kuwaita watoto wao.

Malezi[hariri | hariri chanzo]

Jogoo anapopata chakula huwaita kuku wengine na kuwapa fursa ya kula kwanza. Hufanya hivi kwa kulia kwa mlio wa juu na kuinua chakula na kukiangusha tena mara kadhaa, jogoo hueleza mbele ya temba wake, kwa kumzunguka huku bawa moja likiwa chini na kucheza huku huamsha ubongo wa temba na jogoo huendelea na kazi ya kumzalisha temba huyo.

Uzazi[hariri | hariri chanzo]

Mayai

Kuku hutaga mayai mpaka yanapoisha kwenye mfuko wake. Kisha huanza kutamia. Wakati huu kuku hutulia kwenye kiota chake bila ya kutembea wala kula, huku tu akigeuzageuza mayai yake, akijitahidi kuweka kiwango sawa cha joto na unyevu kwa mayai yote.

Huchukua kwa wastani siku 21 tu mpaka mayai kuanguliwa. Mayai huanza kukomaa mara tu baada ya kuanza kutamiwa. Wakati wa kuanguliwa, kuku husaidia kuvunja mayai taratibu na kuwasaidia vifaranga kutoka. Kuku kwa kawaida, hukaa kwenye kiota kwa siku mbili baada ya kuangua mayai yake. Mayai yote ambayo hayakurutubishwa na jogoo, hayataanguliwa. Kuku kisha kusubiri kwa siku kadhaa, hukiacha kiota chake. Kuku huwa mkali sana nyakati hizi, na kuwafunika vifaranga mara nyingi ili kuwapa joto. Huwaongoza kwenye chakula na maji, kuwaita kwenye chakula na mara kadhaa huwalisha moja kwa moja. Hukaa nao kwa wiki kadhaa mpaka wawe wakubwa, na pindi wanapokuwa, hupoteza hamu nao na kuanza kutaga nao.

Ufugaji wa kuku[hariri | hariri chanzo]

Zaidi ya kuku bilioni 50 huzalishwa duniani kwa ajili ya chakula, hasa kwa ajili ya nyama na mayai yao. Kwa ujumla, Ulaya hutumia mayai milioni 29 kwa siku.

Kuku kama Chakula[hariri | hariri chanzo]

Roasted chicken.jpg

Nyama ya kuku hupendwa sana, hasa kwa ajili ya ladha yake na bei yake ndogo. Hupikwa kwa namna mbali mbali.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Crystal Clear app babelfish.png Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuku kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.