Indonesia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Republik Indonesia
Jamhuri ya Indonesia
Bendera ya Indonesia Nembo ya Indonesia
Bendera Nembo
Wito la taifa: Bhinneka Tunggal Ika
(Kijava/Kikawi: Umoja katika tofauti)
Itikadi: Pancasila
Wimbo wa taifa: Indonesia Raya
Lokeshen ya Indonesia
Mji mkuu Jakarta
6°08′ S 106°45′ E
Mji mkubwa nchini Jakarta
Lugha rasmi Kiindonesia
Serikali Jamhuri
Joko Widodo
Jusuf Kalla
Uhuru
Kutangaza
Kutambuliwa
Kutoka Uholanzi
17 Agosti 1945
27 Desemba 1949
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,904,569 km² (16th)
4.85%
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
222,781,000 (4th)
206,264,595
116/km² (84th)
Fedha Rupiah (IDR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
various (UTC+7 to +9)
not observed (UTC+7 to +9)
Intaneti TLD .id
Kodi ya simu +62

-Indonesia ni nchi ya visiwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Iko upande wa Kusini-Mashariki kati ya Bahari ya Uhindi na Pasifiki. Ni sehemu ya funguvisiwa ya Malay.

Indonesia imepakana na Papua Guinea Mpya kwenye kisiwa cha Guinea Mpya, pia na Timor ya Mashariki kwenye kisiwa cha Timor, halafu na Malaysia kwenye kisiwa cha Borneo.

Nchi zilizo karibu ni Australia, Singapore na Ufilipino.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Indonesia ni nchi ya visiwa 18,000 ilhali zaidi ya 6,000 kati ya hivi vinakaliwa na watu.

Visiwa vikubwa vyenye wakazi wengi ni hasa vitano:

Miji[hariri | hariri chanzo]

Wakazi, lugha, utamaduni, dini[hariri | hariri chanzo]

Nchi ina wakazi 238,452,952 (2004) hivyo ina nafasi ya nne kati ya mataifa makubwa duniani. Ni nchi yenye Waislamu wengi kuliko nyingine zote duniani.

Lugha rasmi ni Bahasa Indonesia (Kiindonesia) iliyoundwa katika karne ya 20 kama lugha ya kitaifa kutokana na lahaja ya Kimalay. Nchini nzima kuna lugha za asili zaidi ya 700 (angalia orodha ya lugha za Indonesia).

Idadi kubwa ya wakazi (86 %) wanahesabiwa kuwa Waislamu, 11 % kama Wakristo, 2 % Wahindu na 1 % Wabuddha. Wahindu wako hasa kwenye kisiwa cha Bali.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Visiwa vya Indonesia viliathiriwa na utamaduni wa Uhindi. Kisiasa palikuwa na falme nyingi.

Tangu karne ya 17 Waholanzi walianza kujenga vituo na kueneza utawala wao. Waliita koloni lao "Uhindi wa Kiholanzi" ("Nederlands-Indië").

Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia Japani ikatwaa visiwa na kuwafukuza Waholanzi. Mwisho wa vita kiongozi Sukarno akatangaza Indonesia kama nchi huru. Waholanzi walijaribu kurudisha utawala wao lakini walilazimishwa na Marekani kukubali uhuru wa nchi.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Indonesia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.

Kigezo:Link FA

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA