Funguvisiwa la Malay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Wallace's line kati ya Australia na Asia Kusini Mashariki inatenganisha maeneo yenye wanyama tofauti. Lombok Strait kati ya visiwa vya Bali na Lombok ilitenganisha maeneo hayo mawili wakati uwiano wa bahari ulikuwa wa chini hivi kwamba visiwa vya kila upande vilikuwa vinafikiwa kwa miguu.

Funguvisiwa la Malay (kwa lugha kubwa za wenyeji: Kepulauan Melayu/Nusantara, Kapuluang Malay, Kapupud-ang Malay) ni funguvisiwa lililoko kati ya Indochina na Australia[1].

Ni zaidi ya visiwa 25,000 vinavyopatikana katika Bahari ya Hindi na Pasifiki na vinavyounda funguvisiwa kubwa kuliko yote duniani, ingawa kwa idadi ya visiwa ni la nne tu.

Watu zaidi ya 380,000,000 wanaishi juu yake, na nchi za Brunei, Singapore, Malaysia Mashariki, Indonesia, Ufilipino na Timor Mashariki ziko katika funguvisiwa hilo.[2]

Visiwa vikubwa zaidi ni: New Guinea, Borneo, Sumatra, Sulawesi na Java huko Indonesia; pamoja na Luzon na Mindanao huko Ufilipino.

Funguvisiwa hilo ni kati ya sehemu za dunia zenye volikano hai zaidi duniani.

Hali ya hewa ni ya kitropiki kutokana na ikweta kupita katikati ya eneo hilo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Wallace, Alfred Russel (1869). The Malay Archipelago. London: Macmillan and Co, 1. 
  2. Encyclopædia Britannica. 2006. Chicago: Encyclopædia Britannica, Inc.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Funguvisiwa la Malay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Majiranukta kwenye ramani: 2°56′S 107°55′E / 2.933°S 107.917°E / -2.933; 107.917