Nenda kwa yaliyomo

Ufilipino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Philippines)
Jamhuri ya Ufilipino
Republika ng Pilipinas (Kifilipino)
Kaulimbiu: Maka-Diyos, Maka-tao, Makakalikasan at Makabansa (Kifilipino)
"Kwa ajili ya Mungu, Watu, Mazingira, na Taifa"
Wimbo wa taifa: "Lupang Hinirang"
Mahali pa Ufilipino
Mji mkuu
na mkubwa
Metro Manila (kwa vitendo)
Lugha rasmiKifilipino, Kiingereza
Lugha ya taifaKifilipino
Kabila (2020)
  • 26.0% Watagalogi
  • 14.3% Wabisaya
  • 8.0% Wailocano
  • 8.0% Wacebuano
  • 7.9% Wailonggo
  • 6.5% Wabikol
  • 20.3% Wengine
Dini (2020)
 • Rais
Bongbong Marcos
Sara Duterte
Uhuru kutoka Hispania na Marekani
 • Tangazo la Uhuru
12 Juni 1898
 • Kukabidhiwa rasmi
11 Aprili 1899
 • Utawala wa kujitegemea
15 Novemba 1935
 • Kutambuliwa rasmi
4 Julai 1946
Eneo
 • Jumlakm2 300,000 (ya 72)
 • Maji (asilimia)0.61%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2024114,163,719
 • Msongamano363.45/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
 • Jumla$1.477 trilioni
 • Kwa kila mtu$12,913
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
 • Jumla$507.670 bilioni
 • Kwa kila mtu$4,439
HDI (2023) 0.720
- juu
Gini (2021)40.2
SarafuPeso ya Ufilipino (PHP)
Majira ya saaUTC+8
Msimbo wa simu++63
Jina la kikoa.ph

Ufilipino, rasmi kama Jamhuri ya Ufilipino (Republika ng Pilipinas Kitagalog), ni nchi ya visiwa iliyoko Asia ya Kusini-Mashariki, katika Bahari ya Pasifiki magharibi.Ufilipino ina idadi ya watu takriban milioni 113, na inashika nafasi ya 13 kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani. Filipino inaundwa na zaidi ya visiwa 7,000 na inapakana na Bahari ya China ya Kusini upande wa magharibi, Bahari ya Pasifiki upande wa mashariki, na Bahari ya Celebes upande wa kusini. Ina jumla ya eneo la takriban kilomita za mraba 300,000, na hivyo kuwa mojawapo ya visiwa vikubwa zaidi duniani. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Manila, ambalo ni sehemu ya mkoa wa Metro Manila, kituo cha kisiasa, kiuchumi, na kitamaduni cha nchi hiyo.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Ufilipino ina visiwa 7,107 vinavyohesabiwa katika makundi matatu yanayoitwa kufuatana na ujirani na visiwa vikubwa vya:

Luzon ni kisiwa kikubwa na Mindanao ni kisiwa cha pili. Visaya ni kundi la visiwa katikati ya funguvisiwa.

Mji mkuu wa Manila uko Luzon. Quezon City ni mji mkubwa. Cebu City ni mji mkubwa upande wa Visaya. Davao City ni mji mkuu wa Mindanao.

Mwaka 1543 nchi iliitwa na Ruy López de Villalobos kwa jina la Kihispania "Las Islas Filipinas" (Visiwa vya Filipo) kwa heshima ya mfalme Filipo II wa Hispania.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wanegritos ni kati ya wakazi asilia ya funguvisiwa hilo, wakifuatwa na Waaustronesia.

Baadaye kukawa na athira ya Wachina, Wamalay, Wahindi na Wamori.

Hispania ilitawala eneo hilo tangu mwaka 1565 hadi Mapinduzi ya Ufilipino ya 1896, ikiacha athari kubwa upande wa dini na utamaduni.

Marekani ilitwaa visiwa hivyo mwaka 1898 katika Vita ya Marekani dhidi Hispania na kuvitawala kama koloni hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati Japani ilipotwaa nchi kwa miaka minne.

Baada ya vita Ufilipino ikapewa uhuru wake.

Siasa na serikali

[hariri | hariri chanzo]

Ufilipino ina serikali ya urais, tena ya umoja (na tofauti kiasi, sababu baadhi ya maeneo yana uhuru mkubwa kutoka serikali ya kitaifa) ambapo Rais ni mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali, pia ni kamanda mkuu wa majeshi. Rais huchaguliwa kwa kura ya umma kwa kipindi kimoja cha miaka sita, wakati ambapo yeye huteua na kusimamia baraza la mawaziri.

Kongamano la bunge limeundwa na Seneti, inayohudumu kama jumba kuu linalo wajumbe waliochaguliwa kwa muda wa miaka sita, na Baraza la Wawakilishi, linalohudumu kama jumba dogo, inayo wajumbe waliochaguliwa kwa muda wa miaka mitatu kutoka kwa wilaya za bunge na kupitia sekta za uwakilishi.

Nguvu za kimahakama zimewekwa katika Mahakama Tukufu iliyoundwa na Jaji Mkuu kama afisa msimamizi, na majaji washirikishi kumi na wanne, wote walioteuliwa na Rais kutoka mapendekezo ya Baraza la Mahakama na Korti.

Kumekuwa na majaribio ya kubadilisha serikali iwe shirikisho, ya bunge kuwa moja au serikali ubunge mwanzo katika muda wa Ramos hadi sasa.

Kuna mikoa ifuatayo:

Wananchi wana asili tofauti sana, kutokana na jiografia na historia ya visiwa hivyo. Mbali na makabila ya wenyeji, kuna Wachina wengi (milioni 2) na machotara wengi sana wenye damu ya Kichina (milioni 18).

Wafilipino milioni 12 wanaishi nje ya nchi.

Wakazi wengi wa Ufilipino hufuata Ukristo wa Kikatoliki (79%) ambao ni urithi wa athira ya Wahispania. Hata hivyo Ufilipino ni nchi isiyo na dini rasmi. Wakristo wengine wanakaribia 10%.

Lugha ya Kiingereza iliachwa na Marekani kama lugha rasmi pamoja na Kifilipino; pia kuna lugha 182 za asili (angalia orodha ya lugha za Ufilipino).

Athira ya Uislamu huonekana hasa kusini mwa kisiwa cha Mindanaoː kwa jumla 5-10% za Wafilipino ni Waislamu wa madhehebu ya Sunni. 2% wanafuata dini za jadi na 1% Ubuddha.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Tovuti rasmi
Biashara
Taarifa za jumla
Vitabu na makala
Wikimedia
Vingine
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufilipino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.