Nenda kwa yaliyomo

Hong Kong

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
中華人民共和國香港特別行政區
Hong Kong 
Eneo lenye utawala wa pekee la Jamhuri ya Watu wa China
Bendera ya Hong Kong Nembo ya Hong Kong
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: sawa na China
Lokeshen ya Hong Kong
Mji mkuu --
Kihistoria makao ya serikali ilikuwa Victoria City.
22°17′ N 114°08′ E
sehemu yenye wakazi wengi wilaya ya Sha Tin
Lugha rasmi · Kichina (lahaja ya Kanton)
Kiingereza
Serikali
John Lee
Ilianzishwa
Kutwaliwa na Uingereza
25 Januari 1841
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,104 km² (--)
4.58
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
7,234,800 (ya 100)
6,708,389
6,544/km² (ya 3)
Fedha Hong Kong dollar (HKD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
HKT (UTC+8)
{{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}})
Intaneti TLD .hk
Kodi ya simu +852 (01 from Macau)

-


Hong Kong

Hong Kong (kwa Kichina: 香港) ni eneo lenye utawala wa pekee ndani ya Jamhuri ya Watu wa China.

Iko upande wa mashariki wa delta ya Mto Zhu Jiang (Pearl River, Mto Lulu) unapoishia katika Bahari ya Kusini ya China. Inatazama bahari ya Uchina upande wa kusini ikipakana na jimbo la Guangdong upande wa kaskazini. Tarehe 23 Oktoba 2018 rais wa China Xi Jinping alizindua rasmi daraja la baharini refu kuliko yote duniani (kilometa 55) linalounganisha Hong Kong, Macau na China bara (mji wa Zhuhai).

Hongkong ilikuwa koloni la Uingereza kwenye pwani ya China kwa zaidi ya miaka 99, likarudishwa chini ya utawala wa Kichina mwaka 1997. Inaendelea kutawaliwa na sheria zake za pekee chini ya mamlaka kuu ya serikali ya Beijing.

Siku hizi ni eneo tajiri kabisa katika Uchina wote.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Baada ya China kushindwa na Dola la Uingereza katika Vita vya kwanza vya Afyuni (1839-1842), Hong Kong ikawa koloni la Uingereza kuanzia Hong Kong Island, ikifuatiwa na Kowloon Peninsula mwaka 1860 na mkataba wa miaka 99 kwa Majimbo Mpya katika 1898.

Baada ya kumilikiwa na Japan wakati wa Vita Kuu ya Pili (1941-1945), Waingereza waliiteka tena hadi Juni 30, 1997.

Kuelekea mwishoni mwa miaka ya 1970, Hong Kong ikawa imara kama mlango mkuu kati ya dunia nzima na China.

Kama matokeo ya mazungumzo kati ya China na Uingereza, Hong Kong ilirudishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China chini ya Azimio la Pamoja la mwaka 1984. Mji ukawa wa kwanza kati ya Mikoa yenye utawala maalumu nchini China tarehe 1 Julai 1997 chini ya kanuni ya "nchi moja, mifumo miwili". Siku hiyo inaitwa 香港回歸 (xiāng gǎng huí guī), kwa Kiswahili "unganisho mpya wa Hong Kong". Jina lingine ni 香港回歸祖國 (xiāng gǎng huí guī zǔ guó), kwa Kiswahili "Hong Kong kurudishwa kwa nchi mama".

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kitovu cha Hong Kong wakati wa usiku

Hong Kong ni maalumu kwa ajili ya mandhari yake pana, bandari asili ya kina na msongamano wa watu (milioni saba na nusu juu ya nchi ya Km² 1108 (sq mi 428). Idadi ya sasa ya wakazi wa Hong Kong inajumuisha 92% ya Wachina asilia. Wengine ni Wafilipino (2.5%), Waindonesia (2.1%) n.k.

Sehemu kubwa ya wakazi wanazungumza Kichina cha Canton (Kikantoni), Hong Kong ikiwa jirani na jimbo la Guangdong, ambalo wafanyakazi wenye ujuzi walikimbia baada ya serikali ya Kikomunisti kuchukua China mwaka 1949 na baadaye husafishwa idadi ya watu mwaka 1960.

Upande wa dini, wengi hawana au wanafuata kidogo jadi, lakini kuna uhuru wa dini mkubwa. 56.1% hawana dini yoyote, Wabuddha na Watao ni 21.3%, Wakristo ni 12% (6.5% Waprotestanti na 5.1% Wakatoliki), Waislamu ni 4%.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Mji una maendeleo makubwa kabisa duniani kama kitovu cha biashara na kituo cha fedha, inachukuliwa kuwa mji katika dunia na mmoja wa Alpha + majiji nane.

Inashika nafasi ya tano katika 2014 Global Miji Index baada ya jiji la New York, London, Tokyo na Paris.

Mji wa kumi kwa kipato cha juu cha kila mwananchi katika dunia, lakini pia inaongozaongoza miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa kwa kukosa usawa wa kipato cha wakazi.

Hong Kong ni ya tatu kama kituo cha biashara muhimu zaidi baada ya New York na London. Huduma uchumi, kwa kodi ya chini na biashara huria, imekuwa huru sana, na fedha yake, dola ya Hong Kong, ni ya 13 kutumika zaidi duniani.

Udogo wa eneo ulileta haja ya miundombinu mingi jirani, na mji ukawa katikati ya vielelezo vya usanifu wa kisasa upande wa majengo, na kuipa Hong Kong mandhari ya mji unaoelekea juu wima.

Hong Kong ina maendeleo makubwa hata upande wa usafiri wa umma duniani ukiwa na mtandao wa asilimia 90, kiwango cha juu zaidi duniani, na inategemea wingi wa watu kupita kwa njia ya barabara au reli.

Uchafuzi wa hewa bado ni mkubwa, viwango vya uzalishaji vikiwa tatizo. Hata hivyo wakazi wa Hong Kong wana matarajio ya kuishi kirefu kuliko watu wengine duniani.

Utalii[hariri | hariri chanzo]

Watalii huenda Hong Kong kwa mvuto wa utamaduni, chakula pamoja na sinema, muziki wa Wachina.

Ingawa Hong Kong ina watu wengi wa matabaka mbalimbali, chakula kwa kawaida huwa kimetokana na utamaduni wa Cantonese au Guangdong cuisine. Wali huliwa kwa wingi pamoja na kuku na mboga zilizotoka mashambani. Chakula huliwa mara tano kwa siku yaani: staftahi, chakula cha mchana, chai ya adhuhuri, chakula cha jioni na siu yeh ambacho ni chakula cha kuliwa kabla uende ukalale.

Mambo ya kuona Hong Kong ni kama vile Kisiwa cha Lantau ambapo kivutio kikubwa ni Giant Buddha, mchongo ulio mkubwa sana wa Buddha, The Peak ambapo utaona Victoria Harbour, Hong Kong Disney Land Resort na Ocean Park Theme.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Biashara
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hong Kong kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.