Milki ya Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Dola la Uingereza)
Rukia: urambazaji, tafuta
Ramani ya nchi ambazo awali zilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza mnamo mwaka 1921

Milki ya Uingereza lilikuwa milki kubwa ambayo ilijumlisha maeneo ambayo yalikuwa yakimilikiwa na Uingereza. Milki hii ilikuwa himaya kubwa ya kisiasa katika historia, na iliweza kumiliki kilele cha robo ya uso wa dunia.

Zaidi ya watu mamlioni ya 458 yalikuwa chini ya udhibiti wa ufalme. Leo hii, maeneo yake mengi yamo nchi wanachama katika Jumuiya ya Madola.

Kiini cha milki hii ilikuwa utawala wa Uingereza juu ya Uhindi uliotajirisha nchi tawala. Mwanzoni ilikuwa kampuni ya binafsi iliyofanya biashara, baadaye kutwaa maeneo hadi Uhindi yote kuwa mchanganyiko wa koloni na "maeneo lindwa" zilizosimamiwa na washauri Waingereza pembeni ya watawala wa kienyeji.

Katika maeneo mengine Uingereza haukutafuta utawala wa moja kwa moja lakini ilitandaza nyavu ya vituo vya kijeshi na kibiashara juu ya sehemu zote za dunia. Pale ambako wafanyabiashara wa Uingereza walikuwa na maslahi jeshi lilingia kati kuhakikisha ya kwamba wapate faida jinsi ilivyokuwa katika China ambayo haikufanywa kuwa koloni lakini kulazimishwa kuruhusu biashara ya madawa ya ulevi kwa njia ya vita mbili.

Katika karne ya 19 Uingereza ilichukua pia utawala juu ya sehemu kubwa ya Afrika; ingawa serikali ya London ilisita mara nyingi kuchukua maeneo mapya maslahi ya wafanyabiashara na walowezi yalisababisha uenezaji wa himaya yake. Katika robo ya mwisho wa karne ya 19 mashindano kati ya mataifa ya Ulaya yalisababisha kutwaliwa kwa maeneo mengine hasa kwa shabaha nchi nyingine isienee; kwa njia hii Kenya ilikuwa koloni ya Uingereza.

Mwisho wa karne ya 19 Uingereza ilianza kuzipa koloni kadhaa viwango tofauti vya kujitawala kama "dominion" kama idadi ya wakazi Waingereza ilikuwa kubwa; kwa njia hii nchi kama Kanada, Australia, New Zealand na Maungano ya Afrika Kusini zilipata serikali na katiba zao na kiwango cha kujitawala kiliongezeka polepole hadi mfalme au malkia wa Uingereza alikuwa mkuu wa dola wa heshima bila athira juu ya siasa tena.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Uingereza ilikosa nguvu ya kuendelea na utawala juu ya maeneo haya makubwa. Ilipaswa kuzipa koloni zake uhuru, kuanzia Uhindi na Pakistan mwaka 1947 hadi nchi za Afrika tangu 1960.

Koloni kadhaa, hasa nchi za visiwa vidogo, ziliamua kutotafuta uhuru zikaendelea kama Maeneo ya ng'ambo ya Uingereza hadi leo. Koloni ya mwisho iliyorudishwa kwa nchi mama ilikuwa Hongkong mwaka 1997.

Visiwa vya Falkland vilisababisha vita kati ya Uingereza na Argentina mwaka 1982 kwa sababu Argentina inadai visiwa kama mali yake ikapeleka wanajeshi visiwani lakini Uingereza ulidai wakazi wa Falkland wanataka kuendelea kama raia wa Uingereza waliondoa Waargentina kwa nguvu ya kijeshi.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Milki ya Uingereza kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.