Ufalme wa Byzanti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mabadiliko ya eneo la Bizanti au Roma ya Mashariki

Ufalme wa Byzanti (kwa Kigiriki: Βυζαντινή Αυτοκρατορία) ni neno linalotumika kutaja Dola la Roma lilivyoendelea mashariki mwa eneo la Mediteranea katika Zama za Kati, ukiwa na makao yake makuu kwenye mji wa Konstantinopoli ulioitwa pia Bizanti na kutumia lugha ya Kigiriki.

Katika baadhi ya maana, hasa kuhusiana na wakati baada ya kuanguka kwa Dola la Roma katika magharibi na mjini Roma penyewe hujulikana pia kama Dola la Roma Mashariki.

Wabizanti wenyewe walijiona ni bado Dola la Roma likiendelea tu. Watawala walitumia cheo cha "Kaisari" kama awali.

Hata hivyo, kwa wakati mwingi wa historia yake, ulifahamika na wenzao wa Ulaya magharibi kama “Ufalme wa Wagiriki” au “Ufalme wa Konstatinopoli” au "Rhômania".

Lakini majirani wa mashariki kama Waarabu waliendela kuwaita "Waroma" (kwa Kiarabu روم rum).

Bizanti ilipata mapigo mawili makubwa katika historia yake:

Shambulio hili lilisababisha nguvu za ufalme kufifia kabisa. Hata baada ya watawala wa Bizanti kurudi Konstantinopoli walikosa nguvu ya kujihami dhidi ya Waturuki Waosmani walioteka Konstantinopoli mwaka 1453 na kumaliza kabisa Bizanti uliokuwa umetunza urithi wa Roma ya Kale hadi wakati ule.

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufalme wa Byzanti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.