Eneo la ng'ambo la Uingereza
Eneo la ng'ambo la Uingereza ni lolote kati ya maeneo 14 ambayo ni chini ya serikali ya Uingereza lakini si sehemu za nchi.
Kwa Kiingereza yameitwa "British Overseas Territory" tangu ilipotungwa sheria ya mwaka 2002 badala ya jina la awali "British dependent territory" yalivyoitwa tangu mwaka 1981. Kabla ya 1981 yaliitwa "makoloni"
Hali ya maeneo hayo ni tofauti na ile ya Jumuiya ya Madola ambayo ni jumuiya ya hiari ya baadhi ya makoloni ya zamani ya Uingereza na nchi nyingine zilizopenda kujiunga.
Mambo ya kisheria
[hariri | hariri chanzo]Kwa jumla wakazi wa maeneo ya ng'ambo ya Uingereza ni raia wa Uingereza na wana haki kuhamia Uingereza yenyewe. Kila eneo lina bunge lake na uhuru fulani wa kutunga sheria zake.
Visiwa vya mfereji wa Kiingereza (Jersey, Guernsey) na Isle of Man si maeneo ya ng'ambo ya Uingereza bali "maeneo chini ya taji la Uingereza".
Maeneo ya ng'ambo ya Uingereza
[hariri | hariri chanzo]Bendera | Eneo | Mahali | Wito | Eneo | Wakazi | Mji Mkuu |
---|---|---|---|---|---|---|
Anguilla | Karibi | Strength and Endurance | 91 km² (35.1 mi²) |
14,869 | The Valley | |
Bermuda | Atlantiki | Quo fata ferunt (Kilatini: "Kote heri inakotupeleka") | 54 km² (20.8 mi²) |
62,506 | Hamilton | |
Eneo la Uingereza katika Antaktika | Antarctica | Research and discovery | 1,709,400 km² (666,000 mi²) |
50/400 staff | Rothera (kituo kikuu) | |
Eneo la Uingereza katika Bahari Hindi | Bahari Hindi | In tutela nostra Limuria (Kilatini: "Tumekabidhiwa Limuria") | 60 km² (23 mi²) |
3,000 military and staff | Diego Garcia (kituo cha kijeshi) | |
Visiwa vya Virgin vya Uingereza | Karibi | Vigilate (Kilatini: "Mwe macho!") | 153 km² (59 mi²) |
31,758 | Road Town | |
Visiwa vya Cayman | Karibi | He hath founded it upon the seas | 264 km² (101.9 mi²) |
68,076 | George Town | |
Visiwa vya Falkland | Atlantiki | Desire the right | 12,173 km² (4,702 mi²) |
3,377 | Stanley | |
Gibraltar | Ulaya ya Kusini | Nulli expugnabilis hosti (Kilatini: "Haishindwi na adui yeyote") | 6.5 km² (2.5 mi²) |
33,701 | Gibraltar | |
Montserrat | Karibi | 101 km² (39 mi²) |
5,215 | Plymouth | ||
Visiwa vya Pitcairn | Pasifiki | 47 km² (18 mi²) |
50 | Adamstown | ||
Saint Helena, Ascension na Tristan da Cunha | Atlantiki | Loyal and unshakeable | 420 km² (162 mi²) |
5,633 | Jamestown | |
Visiwa vya South Georgia na South Sandwich | Atlantiki | Leo terram propriam protegat (Kilatini: "Simba alinda kwake") | 3,903 km² (1,507 mi²) |
99 staff | King Edward Point/Grytviken | |
Akrotiri and Dhekelia (Kupro) | Mediteraneo (Kupro) | Dieu et mon droit (Kifaransa: "Mungu na haki yangu") | 255 km² (98 mi²) |
7,700 + wanajeshi 8,000 | Episkopi Cantonment | |
Visiwa vya Turks na Caicos | Karibi | One people, one nation, one destiny | 430 km² (166 mi²) |
38,191 | Cockburn Town |
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Foreign and Commonwealth Office- "UK Overseas Territories"
- The Commonwealth - UK government site
- Decolonisation - History links for the end of the European formal Empires, casahistoria.net
- UK Overseas Territories Conservation Forum
- British Overseas Territories Act 2002- Text of the Act
- United Kingdom Overseas Territories Association
- Britlink - The British Overseas Territories