Diego Garcia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Location map of Diego Garcia
Kisiwa cha Diego Garcia kwa macho ya ndege

Diego Garcia ni atolli ya Kiingereza katika Bahari Hindi. Ni sehemu ya funguvisiwa ya Chagos na leo kisiwa cha pekee chenye wakazi ambao ni wanajeshi wa Marekani. Ni kituo kikubwa cha kijeshi cha Marekani katika Bahari Hindi.

Kati ya 1850 na 1965 kisiwa kilikuwa sehemu ya eneo la Morisi. 1965 ilitengwa na Morisi pamoja na funguvisiwa yote. Mwaka 1971 Uingereza ilikodi Diego Gracia kwa jeshi la Marekani. Waamerika walitaka kuwa na kituo cha kijeshi kwenye Bahari Hindi katika mashindano yao na Umoja wa Kisovyeti.

Katika miaka miwili iliyofuata wenyeji wote wa funguvisiwa waliondolewa visiwani. Wakahamishwa na watoto wao wanaishi leo huko Mauritius, Shelisheli na Uingereza. Wengi wao wanapigania haki ya kurudi. Mahakama ya Uingereza iliwaruhusu mwaka 2000 warudi tena lakini serikali imekataa mwaka 2004.

Diego Garcia ilikuwa kituo muhimu katika vita za Marekani huko Afghanistan na Irak. Ndege za kijeshi za aina B-52 zinatoka hapa pamoja na ndege za kubeba petroli.

Marekani ina pia kituo cha manowari zake kisiwani.


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia