Moroko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
المملكة المغربية
Al Mamlakah al Maghribīyah

Ufalme wa Moroko
Bendera ya Moroko Nembo ya Moroko
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: الله، الوطن،الملك
(Allāh, al Waţan, al Malik = Mungu, Taifa, Mfalme)
Wimbo wa taifa: Wimbo la Sharifa
Lokeshen ya Moroko
Mji mkuu Rabat
34°02′ Kas 6°51′ Magh
Mji mkubwa nchini Casablanca
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Ufalme wa kikatiba
Mohammad VI
Driss Jettou
Uhuru
- Kutoka Ufaransa
- Kutoka Hispania

2 Machi 1956

7 Aprili 1956

Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
446,550 km² (ya 56)
Kidogo sana
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
32,725,847 (ya 36)
66.8/km² (96)
Fedha Dirham (MAD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
UTC (UTC+0)
UTC (UTC+0)
Intaneti TLD .ma
Kodi ya simu +212

-

Namba zote bila Sahara ya Magharibi


Ramani ya Moroko - mpaka wa kusini haueleweki kimataifa

Moroko (المغرب), (Ufalme wa Moroko (Kiarabu: المملكة المغربية al-mamlaka al-maghribiya "ufalme wa magharibi") ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Jina la "Moroko" limetokana na mji mkuu wa kale Marakesh. Imepakana na bahari za Atlantiki na Mediteranea; barani imepakana na Algeria na Mauretania.

Maeneo ya Kihispania ya Ceuta na Melilla ni ndani ya eneo la Moroko kwenye pwani la Mediteranea.

Mpaka wa kusini haueleweki vizuri kwa sababu Moroko inadai ya kwamba Sahara ya Magharibi ni sehemu ya eneo lake hali isiyokubaliwa na jumuiya ya kimataifa tangu Moroko ilivamia Sahara ya Kusini mwaka 1975.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la Moroko ni 446,550 km². Sehemu kubwa ni jangwa la Sahara. Watu walio wengi huishi kwenye sehemu za rutba karibu na pwani.

Kuna milima inayofunika maeneo makubwa. Milima ya Rif inaongozana na pwani la Mediteranea yenye mwelekeo kutoka kaskazini-magharibi kwenda kazkazini-mashariki. Milima ya Atlas iko katikati ya nchi kutoka kusini-magharibi kwenda kaskazini-mashariki.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 60 % (Januari 2005) za wakazi milioni 32.7 huishi mjini. Kiasili wakazi wengi ni Waberber na Waarabu, pamoja watu wa asili ya Andalusia (Hispania) na wa Afrika kusini ya Sahara. Waberber ndio wenyeji asilia.

Kaskazini ya nchi ambayo kitovu chake ni Fes ina zaidi tabia ya Kiarabu, kusini ambayo kitovu chake ni Marakesh zaidi ya Kiberber.

Walio wengi sana (99%) ni Waislamu Wasunni, wengine Wayahudi na Wakristo.

Wayahudi waliwahi kuwa wengi kidogo lakini idadi yao imepungua katika miaka ya nyuma kutokana na uhamiaji hata kama hali yao katika taifa ni nzuri kulingana na nchi nyingine za Kiarabu. Wakristo karibu wote ni wa asili ya Kiulaya.

Miji mikubwa[hariri | hariri chanzo]

Mji mkuu ni Rabat mwenye wakazi milioni 1.2. Mji mkubwa ni Casablanca (Kiarabu: الدار البيضاء dar al-baiDa = nyumba nyeupe). Miji yote miwili mikubwa ni miji ya badari.

Pwani la Moroko jinsi inavyoonekana kutoka Hispania kupitia mlango wa bahari wa Gibraltar

Miji mitano mikubwa ni kama ifuatayo (namba za sensa ya 2004):

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Lugha rasmi ya nchi ni Kiarabu. Waberber wengi hasa kaskazini waliacha lugha yao na kutumia Kiarabu alkini walileta maneno yao katika lahaja ya Kiarabu cha Kimaroko.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Makala: Historia ya Moroko

Moroko ya Kale[hariri | hariri chanzo]

Habari za kimaandishi ya kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani ilikuwa nchi ya Waberber waliounda ufalme wa Mauretania ya Kale.

Kaskazini ya nchi ikawa jimbo la Kiroma la "Mauretania Tingitana". Ikaona baadaye uvamizi wa Wavandali.

Uvamizi wa Kiarabu[hariri | hariri chanzo]

Karne ya saba ilileta uvamizi wa Waarabu walioteka nchi na kusababisha Waberber kuwa Waislamu polepole. Wakati wa milki ya khalifa ya Kiabasiya Idris ibn Abdallah (788-791) alikusanya makabila ya Waberber na kuunda milki ya kujitegemea. Hii ilikuwa mwanzo wa Maroko kuwa milki ya Kiislamu ya kujitawala.

Murabitun na Muwahidun[hariri | hariri chanzo]

Wafalme wa Wamurabitun (Almoravi)(1073-1147) na Wamuwahidun (Almohad) (1147-1269) walieneza utawala wao hadi Afrika ya Magharibi na juu ya sehemu kubwa ya Andalusia (Hispania), hata hadi mipaka ya Misri.

Athira ya milki ya Moroko ilipungua baadaye hadi Hispania yote imerudishwa kwa watawala wakristo mwaka 1492; pia utawala kusini ya Sahara haukuendelea. Wareno wa Wahispania waliendelea kuteka miji kwenye pwani za Moroko. Utawala wa Hispania juu ya Ceuta na Melilla ni mabaki ya nyakati zile. Sehemu za nchi zilianza kujitawala bila kukubali tena mamlaka wa juu kwa mfano makabila ya Waberber milimani au miji ya Rabat na Sale iliyounda dola ndogo la Jamhuri ya Bou Regreg katika karne ya 17 BK na kujishughulisha na uharamia.

Waalawi (1666 hadi leo)[hariri | hariri chanzo]

Katika karne ya 17 familia ya Waalawi walishika mamlaka wakaendelea nayo hadi leo. Waliweza kutunza uhuru wa nchi hadi mwanzo wa karne ya 20 BK. Lakini mwanzo wa karne ya 20 Ufaransa na Hispania walimlazimisha mfalme Mulay Abdelaziz kukubali mkataba uliofanya Moroko kuwa kama koloni chini ya nchi hizo mbili.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilidhoofisha Ufaransa pamoja na kuingia kwa wanajeshi Waamerika na Waingereza na ahadi zao za kuleta uhuru tokeo lililohamasisha wazalendo wa Maroko kupigania upya uhuru wa nchi. Baada ya vita Wafaransa walijaribu kukandamiza mwendo huo wakamwondoa Sultani Mohammed V nchini 1953. Ghasia ikaongezeka, Sultani Muhammad V akarudi nchi ikapewa uhuri mwaka 1956.

Utawala wa mwanake Hassan II kuanzia mwaka 1961 uliitwa "miaka ya risasi" kwa sababu mfalme alikataa kukubali utaratibu wa kidemokrasia. Uchaguzi zilikuwa za uwongo wapinzani wakatupwa jela au kuuawa. Hassan II alishinda majaribio mbalimbali za kumpindua. Siasa ya kushikamana na Marekani ilimsaidia mfalme kimataifa lakini baada ya mwisho wa "vita baridi" alilazimishwa na Wamarekani kulegea utawala wake.

Mtoto wake Muhamad VI akawa mfalme kijana 1999 akaanza matengenezo ya kisiasa ya wazi zaidi.


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: