Rwanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Republic of Rwanda (engl.)
République Rwandaise (frz.)
Repubulika y'u Rwanda (Kinyarwanda)
Jamhuri ya Rwanda
Bendera ya Rwanda Nembo la Rwanda
(Details) (Details)
Lugha rasmi Kiingereza, Kifaransa, Kinyarwanda
Mji Mkuu Kigali
Serikali Jamhuri
Rais Paul Kagame
Waziri Mkuu Bernard Makuza
Eneo 26.338 km²
Eneo la Rwanda Kazembe 123.553 km²
Idadi ya wakazi 10.746.311 (Januari 2010)
Wakazi kwa km² 401
Uhuru kutoka Ubelgiji 1 Julai 1962
Pesa Rwanda-Franc
Wimbo wa Taifa Rwanda nziza
Rwanda katika Afrika
Ramani ya Rwanda

Rwanda (kifaransa: Le Rwanda) ni nchi ya Afrika ya Mashariki ikipakana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Tanzania.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa Kigali

Eneo la Rwanda ni nyanda za juu na milima; sehemu kubwa ni mita 1500 juu ya UB. Milima katika kaskazini ya nchi inapanda hadi mita 4507 juu ya UB. Kutokana na ujuu hali ya hewa haina joto kali.

Rwanda imepakana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Tanzania. Mpaka na Kongo ni hasa ziwa la Kivu ambayo ni ziwa mojawapo la bonde la ufa la Afrika ya Mashariki. Mpakani na Kongo na Uganda ndiyo milima ya kivolkeno ya Virunga penye sokwe wa milimani.

Rwanda huitwa nchi ya vilima elfu, (Kifaransa: Pays de Mille Collines; Kinyarwanda: Igihugu cy'Imisozi Igihumbi) hivyo ndivyo sehemu kubwa ya eneo lake inavyoonekana hasa katika magharibi.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji mikubwa zaidi ndiyo: Kigali wakazi 745.261, Butare wakazi 89.800, Gitarama wakazi 87.613, Ruhengeri wakazi 86.685 na Gisenyi wakazi 83.623.(namba za Januari 2005)

Kigali ni mji mkuu penye kiwanja cha ndege cha kimataifa na mahoteli makubwa.

Gisenyi ni mji kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa la Kivu mpakani na Kongo ikiwa jirani na mji wa Goma. Kuna usafiri wa mashua kwenda Kibuye na Cyangugu.

Kibuye ni mji mdogo ufukoni wa Ziwa la Kivu. Pana wavuvu wengi, kituo cha watalii na nyumba za kihistoria za wamisionari. Hadi 1994 Watutsi 250,000 waliishi katika wilaya ya Kibuye lakini tangu uangamizaji wa Watutsi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wamebaki 8000 pekee.

Butare ni kitovu cha kiutamaduni katika kusini ya nchi penye chuo kikuu.

Mimea na wanyama[hariri | hariri chanzo]

Rwanda inatunza mazingira ya pekee duniani penye sokwe wa milimani katika milima ya Virunga. Wako hatarini ya kuangamizwa kutokana na uwindaji na kupanuka kwa mashamba kunakopunguza mazingira wanamoishi.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Banyarwanda, Rwanda na Ruanda: Kuma Banyarwanda 2 milioni hapo Uganda. Rwanda ni watu Watutsi, Hutu, Twa; Watu kweli wa kiafrica, ni 8 milioni. Ruanda-Urundi ni 18 milioni. Wanaongea lugha ya kibantu ya Niger-Congo ya Africa ya Kati.

Makabila[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida vikindi vitatu hutajwa kuwa wakazi wa Rwanda ndio Wahutu, Watutsi, Watwa. Lakini kuna tofauti kali kati ya mawazo kama vikundi hivi ni makabila, mataifa ya pekee au tabaka za kijamii. Hali halisi wanatumia lugha ileile ya Kinyarwanda na utamaduni uleule. Kihistoria wengi wanasema ya kwamba Watwa walikuwa wakazi wa kwanza wakiwa wavindaji, Wahutu ndio wakulima wa kibantu waliopatikana tangu uenezaji wa Wabantu katika Afrika ya kati na mababu wa Watutsi waliingia kama wafugaji wa asili ya kaskazini. Watutsi walikuwa tabaka ya kikabaila pia mfalme alikuwa Mtutsi. Lakini wengine wanaamini ya kwamba vikundi vyote vitatu walijitokeza nchini tu si kama tokeo la hamiaji mbalimbali lakini zaidi kama tabaka zilizotofautiana kikazi: Wakulima, wavindaji na wafugaji waliokuwa pia askari wa mfalme.

Wakati wa ukoloni Wabelgiji walihesabu mnamo mwaka 1931 wakazi wa nchi kama wafuatavyo: 84 % Wahutu, 15 % Watutsi na 1 % Watwa. Kabla ya uhuru ilitokea mara kwanza vita vya wenyewe kati ya makabila iliyosababisha kupungua kwa Watutsi kutokana na mauaji na zaidi Watutsi kukimbilia nchi jirani. Mnamo 1990 asilimia ya Watutsi ilikadiriwa kuwa 9 - 10 %.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka ya 1990 ilileta uangamizaji wa Watutsi waliouawa kwa wingi. Kati ya asilimia 75% hadi90% ya wakazi Watutsi waliuawa katika wiki chache za mwaka 1994. Baada ya mwisho wa vita Watutsi wengi ambao wenyewe au wazazi wao walikuwa wamekimbilia Uganda na Tanzania walirudi tena Rwanda.

Demografia[hariri | hariri chanzo]

Kwa wastani kuna wakazi 300 kwa kilomita ya mraba ambayo ni msongamano mkubwa kabisa katika Afrika. Karibu nusu ya wakazi ni watoto hadi ya umri wa miaka 14. Wastani ya muda wa maisha ni miaka 40 pekee. Vita imesababisha idadi kubwa ya wagonjwa wa UKIMWI.

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya kitaifa na lugha ya mama kwa Warwanda wote ni Kinyarwanda ambayo ni lugha ya Kibantu. Mjini na sokoni Kiswahili kinatumika pia lakini si lugha asilia ya Rwanda. Lugha rasmi tangu ukoloni ni Kifaransa. Tangu mwisho wa vita 1994 serikali mpya iliyoongozwa na Watutsi walioishi miaka mingi Uganda imetumia pia Kiingereza kama lugha rasmi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tazama makala "Historia ya Rwanda"

Rwanda ilikuwa ufalme tangu karne ya 16 Rwanda Rugali. Mwanzo wa karne ya 20 ilikuwa sehemu ya Africa ya Mashariki na muzozo wa Wagermani na Ubelgiji. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Rwanda ikawa na vita na Ubelgiji. Uhuru katika mwaka 1961 ilifika pamoja na vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Wahutu na Watutsi. Uhusiano kati ya vikundi hivi viwili uliendelea kuwa vigumu. Kuuawa kwa rais Habariyama mwaka 1994 kulisababisha mauaji ya watu karibu ya milioni moja(~600,000)au Maafa. Kikundi cha RPF chini ya Paul Kagame kilingia kati na kuchukua madaraka. Kwa mwaka wa 2011 Rais D.Gasangwa wa chama cha C.U.D. alipata mamulka ya kiongozi wa Rwanda(Rwanda-EACU) na kuteteya Paul Kagame, kama vyiongozi wa peke ambaye walindaria madiini ya kanisa ya kimethodisti ya kiafrica, kingozi na kiocha.

Rwanda Kazembe ni jimbo muhimu la Congo Zaire. Lugha ya Kiswahili ina zungumunzwa; Kindu, Kisangani , Kalemie, Lubumbashi, Goma, Bunia na Bukavu. Kuna idha ya kiswahili ya Nyota Tv hapo Lubumbashi. Historia ya Rwanda hapa ni kama historia ya Congo. Vita vya Kongo na Deutchlund (Ubelijigi na Ufransa) virikuwa hapa na majeshi ya kimataifa (Kivu Conflict). Vita hivyo virimarizika mwaka wa 2012. Rwanda, Congo Zaire, Uganda na Tanzania wanashirikia kwa umoja wa Africa kwa maendeleo muhima bara Africa kama; elimu, afya, na masoko mbali mbali. Rwanda-EACU ni kiongozi wa umoja wa Africa Mashariki.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Tangu ushindi wake wa kijeshi mwaka 1994 RPF walianzisha serikali ya umoja wa kitaifa. 2003 palitokea uchaguzi wa kwanza.

Serikali[hariri | hariri chanzo]

Raisi na mkuu wa dola ndiye jenerali Paul Kagame (RPF). Waziri Mkuu ndiye Bernard Makuza. Rwanda inataka kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki iritetewa na EACU (Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi); Kuanzia 0013 iripata mamulaka ya jumuiya ya kiafrica, ikiwa kwenye mukatabo wa uchumi wa SADEC.

Utawala - Majimbo[hariri | hariri chanzo]

Tangu 2014 kuna majimbo 11:

 • Byumba
 • Ruhengeri
 • Gitarama
 • Nyanza
 • Goma
 • Beni
 • Kamanyola
 • Kazembe
 • Kamina
 • Fizi
 • Idjwi
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rwanda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia