Nenda kwa yaliyomo

Historia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wanahistoria)
Maktaba ya Aleksandria, Misri ya kale.

Historia (kutoka Kigiriki *ἱστορία, historia*; pia "tarehe" kutoka Kiarabu *تاريخ, tārīkh* kwa maana ya "historia"; na pia hujulikana kama "mapisi" katika baadhi ya lahaja) ni somo linalojihusisha na uchunguzi wa maisha ya binadamu na maendeleo ya jamii zao katika wakati uliopita. Historia inahusu matukio, watu, tamaduni, taasisi, na mabadiliko ya kijamii yaliyotokea kwa nyakati mbalimbali, na hujaribu kuyaeleza kwa kutumia ushahidi uliopo. Somo hili huangazia si tu lini na wapi jambo fulani lilitokea, bali pia kwa nini lilitokea, jinsi lilivyotokea, na athari zake kwa jamii za wakati huo na vizazi vilivyofuata. Historia hutumika kama njia ya kuelewa muktadha wa sasa kwa kuchunguza mwenendo wa matukio ya zamani na kuchota mafunzo kutoka kwao. Kwa msingi huu, historia siyo tu kumbukumbu ya matukio, bali ni zana ya kufasiri maendeleo ya binadamu kwa mapana yake.

Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu").

Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake.

Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani.

Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani (vita, uhuru, viongozi na mengineyo) zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi.

Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka maandishi ya zamani (hasa kwa historia andishi), kutoka fasihi simulizi na kutoka akiolojia (hasa kwa historia ya awali).

Kurasa zinazohusiana

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.