Fasihi simulizi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na maandishi kama kwenye fasihi andishi) kama njia kuu maalum kwa ajili ya kufikisha ujumbe. Ni sehemu ya msingi ya utamaduni, na vipengele vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa jumla.

Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo mdomo kwa mdomo—kwa mfano utenzi, ngano au nyimbo za jadi—hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi.

Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani, k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi. Hata hivyo, mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake haiendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi.


Tanzu na vipera vya Fasihi Simulizi
Hadithi Ushairi Semi Maigizo
Ngano Mashairi Methali Matambiko
Vigano Tenzi Nahau Majigambo
Soga Tendi Misemo Mivigha
Visakale Ngonjera Mafumbo Utani
Visasili Nyimbo Vitendawili Vichekesho
Hekaya Maghani Mizungu Ngoma
Harafa Michezo ya jukwaani
Michezo ya watoto
Ngonjera


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]