Majadiliano:Fasihi simulizi
Hadithi simulizi
Fasihi simulizi
[hariri chanzo]Fasihi simulizi ni aina ya fasihi inayotumia masimulizi ya mdomo katika uwasilishwaji wake.
Dhima za fasihi simulizi
Kuelimisha jamii, Kuburudisha, Kutunza utamaduni na historia ya jamii, Kukuza lugha, Kukomboa jamii,
Tanzu za fasihi simulizi
Fasihi simulizi ina tanzu kuu nne tanzu hizo ni 1.Hadithi 2.Semi 3.Ushaili 4.Sanaa za maonyesho
1.Hadithi
Ni tungo zafasihi simulizi zitumiazolugha ya ujazo ya maongezi ya kila siku, masimulizi hayo hupangwa katika mtiririko wa vituko unaokamilisha kisa.Ili kisa kikamilike katika hadithi,hadithi huwa nawahusika kama vile binadamu na wanyamaambao ndio ni nyenzo ya kukiendesha kisa chenyewe .
2.Semi
Ni fungu la tungo za fasihi simulizi ambazo ni fupifupi zenye kutumia picha,tamathali za semi na ishara.
3.Ushaili
Ni fungu la fasihi simulizi linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo kwa utaratibu maalumu.
4.Sanaa za maonyesho au sanaa za maigizo
Ni zinazoambatana na utendaji wa vitendo vya wahusika mbele ya hadhira.Mfano michezo ya majukwaani.
Asili ya fasihi simuulizi ni ipi?
[hariri chanzo]majibu tafadhari 41.93.80.33 08:50, 22 Machi 2023 (UTC)