Nenda kwa yaliyomo

Michezo ya jukwaani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchezo wa jukwaani chuo kikuu cha Ghana

Michezo ya jukwaani ni michezo ambayo huigizwa katika jukwaa. Michezo ya jukwaani yaani waigizaji huiga maisha halisi ya jamii. Katika michezo ya jukwaani, waigizaji (fanani) huwa mbele ya hadhira na kuonesha matendo mbalimbali yanayoakisi jamii kupitia sanaa hiyo ya maigizo.

Sanaa hiyo ya maigizo huwa na faida kubwa kwa jamii. Baadhi ya faida hizo ni:

(i) Kuburudisha - Katika tamaduni nyingi za Kiafrika na hata nje ya Afrika michezo ya jukwaani huwa inaburudisha hadhira kwa kiasi kikubwa. Watu wanaotazama michezo hiyo hufurahishwa kutokana na matendo ya wahusika, kwa kuwa matendo ya wahusika yamejaa vichekesho, kebehi na chuku nyingi.

(ii) Kuelimisha - Michezo ya jukwaani huelimisha jamii. Hii ni kutokana na sababu kwamba matendo wanayoyaigiza wahusika ni matokeo ya tabia tulizokuwa nazo wanadamu. Wahusika wanaweza kuigiza mamo ambayo yana athari kubwa kwa jamii. Mfano, wizi, uongo, rushwa na kadhalika. Kitendo cha kuigiza matendo hayo na kuyaweka kama ni mambo hasi kwa jamii, husaidia jamii kuachana na mambo hayo.

Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Michezo ya jukwaani kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.