Michezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mashindano ya mbio

Michezo ni amali au mazoezi ya kimwili ambayo mara nyingi yana upande wa mashindano ndani yao. Yanatendeka kufuatana na kawaida na taratibu maalumu zilizokubaliwa kati ya wachezaji au katika jamii. Kuna pia michezo inayotumia vifaa kama vile mpira, silaha, baisikeli, maboti n.k.

Mifano ya michezo ni mpira wa miguu, aina za mbio, mashindano ya kuogelea na kadhalika. Michezo mingi hutekelezwa kama mashindano ya makundi. Aina nyingine ni mashindano ya watu mmojammoja.

Watu wengi hupenda kutazama mashindano ya michezo. Tabia hii imekuwa msingi kwa wachezaji wanaotekeleza michezo yao kikazi na kwa malipo.

Tangu kale watu wamekutana kwa mashindano makubwa ya michezo kati ya jamii, makabila au mataifa. Kati ya mashindano mashuhuri hasa ni Michezo ya Olimpiki.