Pikipiki
Pikipiki ni chombo cha usafiri chenye magurudumu mawili kinachoendeshwa kwa nguvu ya injini ama ya mwako ndani ama ya umeme.
Chanzo cha pikipiki kilikuwa baisikeli iliyoongezwa injini.
Injini
[hariri | hariri chanzo]Pikipiki ndogo huwa mara nyingi na injini ya mapigo mawili lakini kubwa huwa na injini za mapigo manne. Mara nyingi ni injini za petroli kuna pia za diseli. Injini za umeme zimeanza kutumiwa juzijuzi tu zinaenea polepole katika nchi zilizoendelea.
Nguvu ya injini hupelekwa kwenda gurudumu la nyuma kwa njia ya mnyororo. Pikipiki kubwa huwa pia na mhimili kutoka injini hadi gurudumu la nyuma.
Uwezo wa pikipiki
[hariri | hariri chanzo]Kwa kawaida pikipiki huendeshwa na mtu mmoja lakini inaweza kuchukua pia abiria mmoja1 au wawili ingawa ni 1 tu anayeruhusiwa. Pikipiki inaweza kusafirisha hata mizigo midogo. Kuna pia mabehewa ya kando yanayoongezwa kando la pikipiki au trela inayovutwa nayo.
Aina za pikipiki
[hariri | hariri chanzo]Pikipiki za barabara sawa (street motorcycle): muundo wa pikipiki hizi huziwezesha kutumia barabara za lami
Pikipiki za barabara za vijijini (off-road bike): hizi huweza kutumia barabara zisizo na ukarabati
Pikipiki za barabara zote (dual bikes): hizi huweza kutumia barabara za lami au za vijiji.
Pikipiki na motokaa
[hariri | hariri chanzo]Pikipiki zilijitokeza wakati ule kama motokaa. Mtu mmoja husafiri kwa gharama kidogo kwa pikipiki kuliko kwa gari. Tofauti na magari pikipiki haina kinga dhidi ya mvua, baridi au joto kali. Lakini pikipiki ni nyepesi na kwa sababu hiyo huwa na mbio kushinda motokaa. Hata hivyo ni hatari zaidi kuitumia kwa sababu dereva hana kinga dhidi ya ajali. Kwa sababu hiyo kuna nguo za kinga kama kofia ya pikipiki na nyingine.
Matumizi ya pikipiki
[hariri | hariri chanzo]Kimsingi pikipiki hutengenezwa kwa kumbeba dereva pamoja na abiria 1.
- Boda boda za pikipiki hubeba abiria kama teksi.
- Pikipiki hutumiwa hasa mjini kubeba mizigo midogo kama spea au barua kati ya ofisi na maduka.
- Migahawa yenye huduma ya kuwapelekea wateja chakula hadi nyumbani husafirisha mara nyingi kwa pikipiki wakipokea maagizo kwa njia ya simu.
- Wakulima wasio na uwezo wa kununua gari hubeba mazao hadi sokoni.
- Katika nchi zilizoendelea watu wenye motokaa hutumia pikipiki mara nyingi kwa burudani au michezo.
Historia ya pikipiki
[hariri | hariri chanzo]Pikipiki ya kwanza iliyotumia petroli na mfumo wa internal combustion iliitwa Daimler Raitwagen na ilitengenezwa na Wajerumani wawili kwa jina Gottlieb Daimler na Wilhelm Maybach mwaka 1885 nchini Ujerumani.
Vita vya kwanza vya dunia vilichangia pakubwa katika uboreshaji wa pikipiki. Wanajeshi waliona kuwa walikuwa wakitumia muda mrefu sana kusafiri kwa miguu au farasi na kwa hiyo, mahitaji ya pikipiki yakaweza mengi. Kampuni ya Harley-Davidson ilijipata ikitumia takribani asilimia hamsini ya wakati wake katika kutengeneza pikipiki za wanajeshi waliokuwa kwenye vita.
Pikipiki za leo
[hariri | hariri chanzo]Hivi leo, utengenezaji wa pikipiki umechukuliwa sana na Wahindi pamoja na Wajapani. Nchi za Afrika na Asia zimekuwa zikinunua pikipiki kwa wingi kwa minajili ya usafiri haswa kwenye barabara zisizo lami, zenye mawe ambako magari hayawezi yakapenya. Hizi pikipiki za porini huweza kusafiri katika mazingira magumu, kutumia mafuta yasiyo mengi na kupenya vijijini visivyo na barabara nzuri (zenye makorongo na mawe)
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Pikipiki zinatusaidia Sana huku Africa kwa sababu hatuna uwezo wa kununua magari
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |