Baisikeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Baisikeli ya kwanza ilivyobuniwa na Drais
Baisikeli za zamani
Baisikeli ya kisasa
Njia ya pekee kwa baisikeli
Aina ya baisikeli

Baisikeli (kutoka Kilatini "bis", "mara mbili" na Kigiriki "κύκλος", kiklos, duara kupitia Kifaransa/Kiingereza bicycle) ni chombo cha usafiri kinachoendeshwa kwa nguvu ya misuli ya binadamu.

Baisikeli huwa na magurudumu mawili yanayoshikwa na fremu, kiti kimoja, kanyagio, breki na usukani. Tabia nyingine za kawaida ni taa za mbele na nyuma.

Kwa kawaida nguvu hupelekwa kwa nyororo kutoka kanyagio kwenda gurudumu la nyuma. Magurudumu huwa na matairi yaliyojaa hewa. Baisikeli bora huwa pia na gia zinazorahisisha kazi ya kukanyaga kanyagio.

Katika nchi nyingi basikeli ni chombo muhimu cha usafiri. Zamani baisikeli ilikuwa usafiri wa maskini lakini pia katika nchi kadhaa zilizoendelea watu hutumia baisikeli ama kwa usafiri wa mjini au kwa burudani.

Sayansi imegundua ya kwamba baisikeli ni usafiri wa haraka mjini katika umbali wa kilomita chache. Katika nchi nyingi kuna njia za pekee kwa ajili ya baisikeli kando ya barabara ya magari.

Baisikeli ni usafiri unaotumia nishati kidogo na hivyo kuwa nafuu kwa hifadhi ya mazingira.

Mashindano ya baisikeli ni tawi muhimu la michezo ya kimataifa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Baisikeli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.