Nguruwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nguruwe
Nguruwe mweusi (Hylochoerus meinertzhageni)
Nguruwe mweusi (Hylochoerus meinertzhageni)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili))
Nusuoda: Suina (Wanyama kama nguruwe)
Familia: Suidae (Wanyama walio na mnasaba na nguruwe)
Ngazi za chini

Jenasi 6, spishi 19:

Kutoka Wikipedia, ensaiklopidia huru

Nguruwe ni wanyama wa familia Suidae. Nguruwe-kaya hufugwa kote duniani. Spishi mbili zinaitwa ngiri.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia[hariri | hariri chanzo]

Maelezo na tabia[hariri | hariri chanzo]

Nguruwe ana pua kubwa, macho madogo na mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi, uliopinda au ulionyooka. Huwa ana mwili mkubwa, miguu mifupi na nywele zilizojiviringisha. Ana kwato nne kwa kila mguu, huku mbili kubwa za mbele zikitumika kutembelea.[1]

Kuzaa huwezekana msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropiki, lakini hasa misimu ya mvua. Nguruwe jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8 mpaka 18. Kisha ataanza kupata hedhi kwa muda wa siku 21 kama hajashika mimba. Nguruwe dume huweza kushiriki masuala ya uzazi katika umri wa miezi 8 mpaka 10.[2] Kwa uzao mmoja, wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12, waitwao vibwagala. Kisha kuachishwa kunyonya, familia mbili au tatu zinaweza kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa kujamiiana.

Nguruwe hawana tezi za jasho, hivyo nguruwe hujipoza kwa kutumia maji au matope wakati wa joto kali. Pia hutumia matope kama njia ya kujikinga na kuunguzwa na jua. Zaidi, matope huzuia wasiathiriwe na inzi na vijidudu.

Nguruwe wanaofugwa nyumbani hukuzwa na wakulima kwa ajili ya nyama na ngozi. Nywele zao ngumu hutumika pia kwa kutengeneza brashi. Baadhi ya spishi za nguruwe, kama vile wale wa Asia, "pot-bellied pig", huwekwa kama wanyama wa ndani wapenzi.

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Nguruwe ni omnivora, yaani wanakula nyama na majani. Nguruwe hula mabaki na hujulikana kwa kula chakula chochote, kujumuisha wadudu, minyoo, magamba ya miti, takataka na hata nguruwe wengine. Wakiwa mwituni hula majani, nyasi, mizizi, matunda na maua. Kwa nadra, nguruwe wakiwa wanafugwa, huweza kula watoto wao kama wakichukizwa sana.

Nguruwe wa kawaida wana kichwa kikubwa chenye pua ndefu iliyoimarishwa kwa mfupa mgumu na mduara wa tishu ngumu mbele. Pua hiyo hutumika kuchimba udongo ili kutafuta chakula na ni ogani yenye uwezo mkubwa wa kuhisi.

Nguruwe huwa na seti kubwa ya meno 44. Meno ya nyuma yametoholewa kusaga, na huendelea kukua na huchongwa na misuguano ya meno yenyewe.

Nguruwe wanaochungwa mwituni kwa msaada wa wachungaji, wana uwezo mkubwa wa kunusa, na hutumika kutafuta uyoga katika nchi nyingi za Ulaya.

Nguruwe wafugwao[hariri | hariri chanzo]

Mkulima wa Swideni na kitoto cha nguruwe (kibwagala) mapema karne ya 20.

Nguruwe wa nyumbani hutambulika kwa jina la kisayansi Sus scrofa. Walianza kufugwa karibu miaka 5,000 mpaka 7,000 iliyopita. Walizaliwa na rangi ya kahawia na kuendelea kuwa wa kijivu. Meno chonge ya juu huwa kama ndovu za kipekee zilizopinda nje na kuelekea juu. Urefu wa nguruwe huweza kufikia milimita 900 – 1800 na uzito wa kg 50 – 350.

Nguruwe wana akili na huweza kufundishwa kazi na mbinu ndogondogo. Hivi karibuni, wamefurahia kupewa nafasi kama wanyama kipenzi wa ndani na, hasa wale nguruwe wadogo.

Nguruwe na tamaduni[hariri | hariri chanzo]

Nguruwe mara nyingi hutumiwa kwenye utamaduni na ni mada maarufu kwenye misemo na nukuu maarufu.

Nguruwe kwenye dini[hariri | hariri chanzo]

Mchoro wa Mt. Anthony na michoro ya nguruwe nyuma yake.
  • Kwa dini ya Wahindi mungu Vishnu alichukua umbo la nguruwe dume Varaha kwa ajili ya kuokoa dunia na pepo aliyekuwa ameivuta mpaka kilindini mwa Bahari.
  • Nguruwe ni mmoja kati ya mzunguko wa wanyama 12 ambao wanatokea kwenye kalenda ya kichina ya "Chinese zodiac". Waamini wa elimu ya anga wanaamini kila mnyama ana maana fulani pekee.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.