Gurudumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Magurudumu ya ubao

Gurudumu ni mtambo mwenye umbo la duara. Linaruhusu gari kutembea; magurudumu yanazunguka na mzigo (mfano gari) juu yake unaenda mbele kwa kutumia nguvu kidogo.

Gurudumu linapunguza msuguano; badala ya msunguano wa kitu chote kinachosogea mbele kwenye ardhi kuna msuguano wa sehemu ndogo ya gurudumu na msuguano wa gurudumu kwenye ekseli yake. Msuguano kati ya ekseli na gurudumu unapunguzwa kwa njia ya kutia mafuta au kuweka beringi gololi kati ya gurudumu na ekseli.

Sehemu kubwa ya usafiri kwenye nchi kavu hutegemea magurudumu kwa mfano motokaa, lori, reli ya kawaida na baisikeli. Magurudumu ni pia sehemu kubwa ya machine nyingi.

Tangu karne ya 19 magurudumu yanaviringishwa kwa matairi ya mpira na hii inanyosha mwendo wake.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wataalamu wa historia huamini ya kwamba watu wa Babeli walikuwa wa kwanza kugundua gurudumu na kulitumia tangu mwaka 4000 KK. Watu wa China ya Kale waliligundua pia mnamo 2800 KK.

Ustaarabu za Amerika ya Kale kama Inka na Azteki waligundua gurudumu pia likatumiwa kwa vitu vya kucheza watoto lakini halikuwa na matumizi ya kikazi.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gurudumu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.