Nenda kwa yaliyomo

Riksho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Riksha)
Riksho ya kuvutwa
Riksho ya Kihindi
Riksho ya baisikeli ya kisasa katika miji mikubwa nchini Ujerumani inafanya kazi kama teksi kwa umbali mdogo.

Riksho (pia: riksha; kwa Kiingereza: rickshaw; kutoka neno la Kijapani) ni chombo cha usafiri ambacho kiasili kilikuwa gari dogo lenye kiti lililovutwa na mtu, ilhali abiria amekalia nyuma.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Riksho ya kwanza ilitengenezwa mwaka wa 1869 nchini Japani. Taarifa zinatofautiana kama mvumbuzi alikuwa mwenyeji wa Japani au mgeni kutoka Ulaya[1] au Marekani [2].

Zilienea haraka katika nchi za Asia. Riksha za kuvutwa zilipokelewa vizuri mno na watu wa Asia katika karne ya 19 huku vijana wengi wakijitosa katika ajira za kuvuta riksha hizi. Mnamo mwaka 1920 kulikuwa na riksha 60,000 mjini Beijing (China) na takriban mmoja kati ya wanaume sita katika mji huu alifanya kazi ya kuvuta chombo hiki[3].

Baadaye riksho ziliendelea kuunganishwa na baisikeli ilhali dereva moja anaendesha baisikeli ya magurudumu matatu ambako abiria hukalia ama mbele ama nyuma ya dereva. Tangu kuenea kwa pikipiki mfumo huu ulibadilishwa kuwa pia na injini ya petroli. Riksho za pikipiki ziliendelea kupata chumba kidogo cha abiria na hivyo zinajulikana kwa jina la tuk-tuk katika sehemu kadhaa za Asia, pia kwa jina la bajaj nchini Uhindi na kutoka huko zilifika kama "bajaji" katika Afrika ya Mashariki.

Riksho asilia za kuvutwa zinapatikana bado katika miji michache lakini idadi inapungua haraka.

  1. Chi Ming Fung, Reluctant Heroes, uk. 1
  2. Lewis anadai ilianzishwa Marekani na kupelekwa Asia baadaye
  3. Strand, Rickshaw Beijing, uk. 20-21

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.