Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria na Uturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati", ing. central powers) kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa, Urusi, Uingereza, Italia, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano", ing. allied powers).
Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya Kati. Kupitia koloni za Ujerumani ilipiganiwa pia Afrika na Asia ya Mashariki ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa.
Sababu na matokeo
Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani Ulaya na duniani kote.
Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa Milki ya Osmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani.
Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile Chekoslovakia, Ufini, Latvia, Estonia, na Yugoslavia pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo Austria, Hungaria, Lithuania na Poland. Katika Mashariki ya Kati Uturuki ilianzishwa kama nchi mpya, ilhali kipindi kifupi cha ukoloni wa Uingereza na Ufaransa kilianza huko Syria, Iraq na Lebanoni.
Shirikisho la Mataifa liliundwa kama chombo cha kwanza kilicholenga kuunganisha nchi zote za Dunia na kuzuia vita mpya. Koloni za awali za Ujerumani na majimbo ya Kiarabu ya Milki ya Osmani zilidhaminiwa kwa Uingereza na Ufaransa kwa niaba ya Shirikisho, hatua iliyoweka maeneo haya chini ya uangalizi wa kimataifa, tofauti na koloni za kawaida.
Hali kabla ya vita
Sehemu kubwa ya Ulaya iliwahi kuwa na kipindi kirefu cha amani tangu vita kati ya Ufaransa na Ujerumani mnamo 1870-1871. Mataifa ya Ulaya yalikuwa na mfumo wa mikataba na mapatano kati yao yaliyolenga kuhakikisha uwiano wa mataifa. Mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Italia pamoja na milki ya Austria-Hungaria.
Hali ilikuwa tofauti katika Kusini-Mashariki mwa bara hilo. Hadi nusu ya pili ya karne ya 19 sehemu kubwa ya Balkani ilitawaliwa na Milki ya Osmani iliyokuwa milki ya Kiislamu ya kutawala Wakristo wengi. Milki hii iliendelea kudhoofika wakati wa karne ya 19. Nchi mbalimbali zilijitenga na kupata uhuru, kama vile Ugiriki, Serbia, Bulgaria na Romania. Nchi hizi mpya zilipigana kivita kati yao na Milki ya Osmani hadi mwaka 1912.
Mwanzo wa vita
Vita Kuu ilianza kutokana na ugomvi kati ya Austria-Hungaria na Serbia. Kutokana na muundo wa mikataba ya kusaidiana kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo ulisababisha mfululizo wa hali ya vita kati ya mataifa, na mengine ya Balkani yaliyotafuta uhuru wao.
Tarehe 28 Juni 1914 katika mji wa Sarayevo, Bosnia, mwana wa Kaizari wa Austria aliyekuwa mfalme mteule aliuawa pamoja na mke wake na mgaidi Mserbia mwanachama wa kundi la "Mkono Mweusi" lililopinga utawala wa Austria-Hungaria katika Bosnia. Austria iliamuru Serbia ifuate masharti makali katika uchunguzi wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya mwisho ya masharti, Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia tarehe 28 Julai 1914.
Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hiyo: Warusi walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria. Hapo wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano ya usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na mkataba wa kusaidiana na Ufaransa, kwa hivyo hali ya vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani. Ujerumani ilishambulia Ufaransa kwa kuingia Ubelgiji na kupigana na jeshi la nchi hiyo. Mashambulio hayo yalisababisha Uingereza kujiunga na vita dhidi ya Ujerumani.
Japan iliyokuwa na mkataba wa kusaidana na Uingereza tangu mwaka 1902 iliona nafasi ya kukamata koloni za Ujerumani katika Bahari Pasifiki ikaingia upande wa maadui wa Ujerumani.
Kuanzia Oktoba 1914 Milki ya Osmani (Uturuki) ilijiunga na vita kufuatana na mkataba wake wa siri na Ujerumani.
Mwaka 1915 Italia ilijiunga na Wafaransa na Waingereza kwa kushambulia Austria-Hungaria iliyotawala bado maeneo katika kaskazini ya rasi ya Italia, ingawa awali ilikuwa na mkataba na dola hilo.
Vita katika nchi mbalimbali
Vita ilipigwa kwa ukali miaka ya 1914-1918. Wajerumani waliingia ndani ya Ufaransa lakini walikwama kabla ya kufikia jiji kuu la Paris. Kwa muda mrefu mstari wa mapambano ulibaki palepale.
Katika Mashariki Wajerumani na Waaustria walifaulu kurudisha mashambulio ya Kirusi na kuteka sehemu za Urusi.
Katika Kusini mwa Ulaya Waustria walifaulu kwa shida kubwa kuteka Serbia na Montenegro pamoja na Albania. Mapigano dhidi ya Italia yalikwama kwenye milima ya Alpi.
Waosmani walishindwa kwa ujumla katika mashambulio yao dhidi ya Warusi katika eneo la Kaukazi na dhidi ya Waingereza katika Misri. Lakini walifaulu kuzuia Waingereza wasifike Uturuki penyewe. Waingereza walipeleka jeshi katika Irak ya kusini wakafaulu kuwarudisha Waosmani hadi kaskazini ya nchi hii.
Vita katika koloni
Tazama makala kuu: Vita Kuu ya Kwanza katika Afrika ya Mashariki
Vita ilienea haraka baharini na katika koloni za Ujerumani zilizovamiwa na Waingereza, Wafaransa, Afrika Kusini na Japani. Koloni hizo zilikuwepo Afrika na kwenye visiwa vya Pasifiki pamoja na China. Ujerumani ilikuwa na vikosi vya kijeshi katika koloni za Afrika na pia huko Qingdao nchini China.
Kwa ujumla koloni zote zisizokuwa na jeshi zilitekwa na mataifa ya ushirikiano bila mapigano.
- Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani ilivamiwa na Afrika Kusini na jeshi la ulinzi la Kijerumani likajisalimisha mnamo Julai 1915.
- Kamerun ilivamiwa na Ufaransa na Uingereza kutoka koloni zao za Nigeria na Afrika ya Kati ya Kifaransa. Wajerumani wakajisalimisha katika Februari 1916.
- Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilikuwa mahali pa mapigano yaliyoendelea kwa miaka yote ya vita. Jeshi la Ulinzi la Kijerumani lililoitwa Schutztruppe chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck lilifaulu kutetea eneo la koloni dhidi ya mashambulio ya kwanza ya Waingereza kutoka Kenya hadi 1916. Kwenye Novemba 1914 jeshi la askari 8,000 kutoka Uhindi lilishindwa kwenye mapigano ya Tanga. Hadi mwanzo wa 1916 Waingereza walikusanya jeshi kubwa kutoka Afrika Kusini na Uhindi wakafaulu kutwaa sehemu kubwa ya koloni hadi Agosti 1916. Jeshi la Schutztruppe likaendelea kushika sehemu ya kusini ya koloni hadi 1917 ilipopaswa kuhamia eneo la Kireno katika Msumbiji. Waingereza na Wareno walishindwa kulishika kundi la Kijerumani. Mwaka 1918 Lettow-Vorbeck alirudi Tanganyika akaingia Rhodesia ya Kaskazini alipoambiwa na Waingereza mnamo Novemba 1918 ya kwamba vita ya Ulaya ilikwisha tayari.
Mwisho wa vita
Wakati 1917 mataifa ya Ulaya yalionyesha dalili za uchovu. Katika hali hiyo mabadiliko mawili makubwa yalitokea: Marekani ilijiunga na vita dhidi ya Wajerumani na Urusi ilikuwa na mapinduzi yaliyolazimisha serikali mpya kutia sahihi mapatano ya kumaliza vita dhidi ya Ujerumani iliyoteka maeneo makubwa ya Urusi.
Nguvu ya Marekani ilionekana haraka na bahati ya Ujerumani ilipungua sana. Austria-Hungaria ilidhoofishwa vilevile.
Mwaka 1918 iliona mwisho wa vita. Jeshi la Kiosmani lilishindwa hadi serikali ya milki kuomba kusimamishwa kwa vita. Mataifa ya ushirikiano yalikaribia mipaka ya Ujerumani na hapo mgomo wa wanamaji ilifuatwa na migomo ya wafanyakazi katika viwanda vikubwa iliyosababisha mapinduzi yaliyoangusha serikali ya Kaisari Wilhelm II. Migomo ya wanajeshi ililazimisha Austria-Hungaria kuomba kusimamisha vita.
Milki za Austria na Uturuki zilikwisha zikagawiwa na sehemu zao zilikuwa nchi mpya au nchi zilizoundwa upya.
Mkutano wa Paris
Mwaka 1919 mataifa washindi walikutana Paris (Ufaransa) wakikubaliana masharti ya kumaliza hali ya vita dhidi ya Mataifa ya Kati. Mikataba mbalimbali iliandaliwa kati ya washindi na kuwekwa mbele ya nchi zilizoshindwa.
Mikataba hii ilikuwa:
- Mkataba wa Versailles na Ujerumani (28 Juni 1919),
- Mkataba wa Saint-Germain na Austria (10 Septemba 1919),
- Mkataba wa Neuilly na Bulgaria (27 Novemba 1919),
- Mkataba wa Trianon na Hungaria (4 Juni 1920),
- Mkataba wa Sèvres na Milki ya Osmani (Uturuki) (10 Agosti 1920; ukasahihishwa na mkataba wa Lausanne (24 Julai 1923).
Mkutano wa Paris ulitoa masharti makali dhidi ya Ujerumani katika Mkataba wa Versailles. Ujerumani uliondolowa makoloni yote yaliyokabidhiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa kama maeneo ya kukabidhiwa kwa Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Japani, Afrika Kusini na Australia.
Mkutano wa Paris ulikuwa jaribio la kuunda utaratibu mpya duniani uliotakiwa kulindwa na Shirikisho la Mataifa. Lakini ukosefu wa nguvu kwa upande wa Shirikisho la Mataifa pamoja na kuanza na kupanuka kwa mwendo mpya wa Kifashisti iliyochukua utawala katika Italia na Ujerumani vilishinda nia hiyo.
Wataalamu wasio wachache wanasema mwisho wa vita kuu ya kwanza ulipanda tayari mbegu za Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Ni kwamba Wajerumani na wakazi wa nchi nyingine zilizoshindwa walijiona wamekosewa haki, lakini pia Waitalia walioshinda kwa gharama kubwa ya damu walijiona wamedanganywa kwa kutotimiziwa ahadi walizopewa ili wasaliti Ujerumani na Austria-Hungaria na kuingia vitani upande wa pili. Hivyo vyama vya mrengo wa kulia viliweza kupata nguvu na hatimaye kupanga kisasi.
Vita ya kwanza ya Dunia?
Vita hii ilitwa "Vita ya Dunia" kwa sababu mapigano yalisambaa kote duniani. Sehemu kubwa ya mapigano yalitokea Ulaya na Asia ya Magharibi lakini pia katika makoloni ya Afrika, Asia na Pasifiki. Nchi za Amerika hazikuona mapigano kwenye nchi kavu lakini manowari za Ujerumani zilipigana na mataifa ya ushirikiano mbele ya pwani za Marekani na Amerika Kusini.
Ilikuwa pia vita ya kwanza iliyopigwa kote duniani ilhali habari zake ziliweza kufika katika muda wa masaa au siku chache kwa mataifa yote kutokana na upatikanaji wa vyombo vya mawasiliano hasa simu za kimataifa na redio.
Lakini kwa kweli haikuwa vita ya kwanza ya "Dunia" maana vita ya miaka saba (1756-1762) ilipigwa tayari kwenye mabara yote ya Dunia baina ya nchi zenye koloni, hasa Uingereza, Ufaransa na Hispania.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
- American Battle Monuments Commission (1938), American Armies and Battlefields in Europe: A History, Guide, and Reference Book, US Government Printing Office, OCLC 59803706
- Army Art of World War I, United States Army Center of Military History: Smithsonian Institution, National Museum of American History, 1993, OCLC 28608539
- Bade, Klaus J; Brown, Allison (tr.) (2003), Migration in European History, The making of Europe, Oxford: Blackwell, ISBN 0-631-18939-4, OCLC 52695573 (translated from the German)
- Baker, Kevin (Juni 2006), "Stabbed in the Back! The past and future of a right-wing myth", Harper's Magazine
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Balakian, Peter (2003), The Burning Tigris: The Armenian Genocide and America's Response, New York: HarperCollins, ISBN 978-0-06-019840-4, OCLC 56822108
- Ball, Alan M (1996), And Now My Soul Is Hardened: Abandoned Children in Soviet Russia, 1918–1930, Berkeley: University of California Press, ISBN 978-0-520-20694-6, reviewed in Hegarty, Thomas J (Machi–Juni 1998). "And Now My Soul Is Hardened: Abandoned Children in Soviet Russia, 1918–1930". Canadian Slavonic Papers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-05-09. Iliwekwa mnamo 2014-07-29.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) (via Highbeam.com) - Bass, Gary Jonathan (2002), Stay the Hand of Vengeance: The Politics of War Crimes Tribunals, Princeton, New Jersey: Princeton University Press, ku. 424pp, ISBN 0-691-09278-8, OCLC 248021790
- Blair, Dale (2005), No Quarter: Unlawful Killing and Surrender in the Australian War Experience, 1915–1918, Charnwood, Australia: Ginninderra Press, ISBN 1-74027-291-9, OCLC 62514621
- Brands, Henry William (1997), T. R.: The Last Romantic, New York: Basic Books, ISBN 0-465-06958-4, OCLC 36954615
- Brown, Judith M. (1994), Modern India: The Origins of an Asian Democracy, Oxford and New York: Oxford University Press, ISBN 0-19-873113-2
- Chickering, Rodger (2004), Imperial Germany and the Great War, 1914–1918, Cambridge: Cambridge University Press, ISBN 0-521-83908-4, OCLC 55523473
- Clark, Charles Upson (1927), Bessarabia, Russia and Roumania on the Black Sea, New York: Dodd, Mead, OCLC 150789848, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-08, iliwekwa mnamo 2014-07-29
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Cockfield, Jamie H (1997), With snow on their boots : The tragic odyssey of the Russian Expeditionary Force in France during World War 1, Palgrave Macmillan, ISBN 0-312-22082-0
- Conlon, Joseph M, The historical impact of epidemic typhus (PDF), Montana State University, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2010-06-11, iliwekwa mnamo 21 Aprili 2009
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Cook, Tim (2006), "The politics of surrender: Canadian soldiers and the killing of prisoners in the First World War", The Journal of Military History, 70 (3): 637–665, doi:10.1353/jmh.2006.0158
- Cross, Wilbur L (1991), Zeppelins of World War I, New York: Paragon Press, ISBN 978-1-55778-382-0, OCLC 22860189
- Djokić, Dejan (2003), Yugoslavism : histories of a failed idea, 1918–1992, London: Hurst, OCLC 51093251
- Doughty, Robert A. (2005), Pyrrhic victory: French strategy and operations in the Great War, Harvard University Press, ISBN 978-0-674-01880-8
- Duffy, Michael, Somme, First World War.com, ISBN 0-297-84689-2, iliwekwa mnamo 25 Februari 2007
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Dupuy, R. Ernest and Trevor N. (1993), The Harper's Encyclopedia of Military History, 4th Edition, Harper Collins Publishers, ISBN 978-0-06-270056-8
- Encyclopaedia Britannica (12th ed. 1922) comprises the 11th edition plus three new volumes 30-31-32 that cover events since 1911 with very thorough coverage of the war as well as every country and colony. partly online and list of article titles
- Evans, David (2004), The First World War, Teach yourself, London: Hodder Arnold, ISBN 0-340-88489-4, OCLC 224332259
- Evans, Leslie (27 Mei 2005), Future of Iraq, Israel-Palestine Conflict, and Central Asia Weighed at International Conference, UCLA International Institute, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-24, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Falls, Cyril Bentham (1960), The First World War, London: Longmans, ISBN 1-84342-272-7, OCLC 460327352
- Farwell, Byron (1989), The Great War in Africa, 1914–1918, W.W. Norton, ISBN 978-0-393-30564-7
- Ferguson, Niall (1999), The Pity of War, New York: Basic Books, ku. 563pp, ISBN 0-465-05711-X, OCLC 41124439
- Ferguson, Niall (2006), The War of the World: Twentieth-Century Conflict and the Descent of the West, New York: Penguin Press, ISBN 1-59420-100-5
- Fortescue, Granville Roland (28 Oktoba 1915), "London in Gloom over Gallipoli; Captain Fortescue in Book and Ashmead-Bartlett in Lecture Declare Campaign Lost", New York Times
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Fromkin, David (1989). A Peace to End All Peace: The Fall of the Ottoman Empire and the Creation of the Modern Middle East. New York: Henry Holt and Co. ISBN 0-8050-0857-8.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Fromkin, David (2001), A Peace to End All Peace: The Fall of the Ottoman Empire and the Creation of the Modern Middle East, New York: Owl Books, uk. 119, ISBN 0-8050-6884-8, OCLC 53814831
- Fromkin, David (2004), Europe's Last Summer: Who Started the Great War in 1914?, New York: Alfred A. Knopf, ISBN 0-375-41156-9, OCLC 53937943
- Gelvin, James L (2005), The Israel-Palestine Conflict: One Hundred Years of War, Cambridge: Cambridge University Press, ISBN 0-521-85289-7, OCLC 59879560
- Grant, R.G. (2005), Battle: A Visual Journey Through 5,000 Years of Combat, DK Publishing, ISBN 978-0-7566-5578-5
- Gray, Randal; Argyle, Christopher (1990), Chronicle of the First World War, New York: Facts on File, ISBN 978-0-8160-2595-4, OCLC 19398100
- Gilbert, Martin (1994), First World War, Stoddart Publishing, ISBN 978-0-7737-2848-6
- Gilbert, Martin (2004), The First World War: A Complete History, Clearwater, Florida: Owl Books, uk. 306, ISBN 0-8050-7617-4, OCLC 34792651
- Goodspeed, Donald James (1985), The German Wars 1914–1945, New York: Random House; Bonanza, ISBN 978-0-517-46790-9
- Gray, Randal (1991), Kaiserschlacht 1918: the final German offensive, Osprey, ISBN 978-1-85532-157-1
- Green, John Frederick Norman (1938), "Obituary: Albert Ernest Kitson", Geological Society Quarterly Journal, 94, Geological Society
- Halpern, Paul G (1995), A Naval History of World War I, New York: Routledge, ISBN 1-85728-498-4, OCLC 60281302
- Harris, J. P. (2008), Douglas Haig and the First World War (tol. la 2009), Cambridge: CUP, ISBN 978-0-521-89802-7
- Hartcup, Guy (1988), The War of Invention; Scientific Developments, 1914–18, Brassey's Defence Publishers, ISBN 0-08-033591-8
- Havighurst, Alfred F (1985), Britain in transition: the twentieth century (tol. la 4), University of Chicago Press, ISBN 978-0-226-31971-1
- Heller, Charles E (1984), Chemical warfare in World War I : the American experience, 1917–1918, Fort Leavenworth, Kansas: Combat Studies Institute, OCLC 123244486, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-07-04, iliwekwa mnamo 2014-07-29
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Heyman, Neil M (1997), World War I, Guides to historic events of the twentieth century, Westport, Connecticut: Greenwood Press, ISBN 0-313-29880-7, OCLC 36292837
- Hickey, Michael (2003), The Mediterranean Front 1914–1923, The First World War, juz. la 4, New York: Routledge, ku. 60–65, ISBN 0-415-96844-5, OCLC 52375688
- Hinterhoff, Eugene (1984), Young, Peter (mhr.), "The Campaign in Armenia", Marshall Cavendish Illustrated Encyclopedia of World War I, juz. la ii, New York: Marshall Cavendish, ISBN 0-86307-181-3
- Hooker, Richard (1996), The Ottomans, Washington State University, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1999-10-08, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008
{{citation}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Horne, John; Kramer, Alan (2001), German Atrocities, 1914: A History of Denial, Yale University Press, OCLC 47181922
- Hovannisian, Richard G. (1967), Armenia on the Road to Independence, 1918, Berkeley: University of California Press, ISBN 0-520-00574-0
- Hull, Isabel Virginia (2006), Absolute destruction: military culture and the practices of war in Imperial Germany, Cornell University Press, ISBN 978-0-8014-7293-0
- Humphries, Mark Osborne (2007), Hayes, Geoffrey; Iarocci, Andrew; Bechthold, Mike (whr.), Vimy Ridge: A Canadian Reassessment, Waterloo: Wilfrid Laurier University Press, ku. 65–85, ISBN 0-88920-508-6
- Inglis, David (1995), Vimy Ridge: 1917–1992, A Canadian Myth over Seventy Five Years (PDF), Burnaby: Simon Fraser University, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-09-16, iliwekwa mnamo 2014-07-29
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Isaac, Jad; Hosh, Leonardo (7–9 Mei 1992), Roots of the Water Conflict in the Middle East, University of Waterloo, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-28, iliwekwa mnamo 2014-07-29
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: location missing publisher (link) - Jenkins, Burris A (2009), Facing the Hindenburg Line, BiblioBazaar, ISBN 978-1-110-81238-7
- Johnson, James Edgar (2001), Full Circle: The Story of Air Fighting, London: Cassell, ISBN 0-304-35860-6, OCLC 45991828
- Jones, Howard (2001), Crucible of Power: A History of US Foreign Relations Since 1897, Wilmington, Delaware: Scholarly Resources Books, ISBN 0-8420-2918-4, OCLC 46640675
- Kaplan, Robert D (Februari 1993), "Syria: Identity Crisis", The Atlantic, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Karp, Walter (1979), The Politics of War (tol. la 1st), ISBN 0-06-012265-X, OCLC 4593327, Wilson's maneuvering US into war
- Keegan, John (1998), The First World War, Hutchinson, ISBN 0-09-180178-8, general military history
- Keene, Jennifer D (2006), World War I, Daily Life Through History Series, Westport, Connecticut: Greenwood Press, uk. 5, ISBN 0-313-33181-2, OCLC 70883191
- Kernek, Sterling (Desemba 1970), "The British Government's Reactions to President Wilson's 'Peace' Note of December 1916", The Historical Journal, 13 (4): 721–766, doi:10.1017/S0018246X00009481, JSTOR 2637713
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Kitchen, Martin (2000) [1980], Europe Between the Wars, New York: Longman, ISBN 0-582-41869-0, OCLC 247285240
- Knobler, Stacey L, mhr. (2005), The Threat of Pandemic Influenza: Are We Ready? Workshop Summary, Washington DC: National Academies Press, ISBN 0-309-09504-2, OCLC 57422232, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-30, iliwekwa mnamo 2014-07-29
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Kurlander, Eric (2006), Steffen Bruendel. Volksgemeinschaft oder Volksstaat: Die "Ideen von 1914" und die Neuordnung Deutschlands im Ersten Weltkrieg (Book review), H-net, iliwekwa mnamo 17 Novemba 2009
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Lehmann, Hartmut; van der Veer, Peter, whr. (1999), Nation and religion: perspectives on Europe and Asia, Princeton, New Jersey: Princeton University Press, ISBN 0-691-01232-6, OCLC 39727826
- Lewy, Guenter (2005), The Armenian Massacres in Ottoman Turkey: A Disputed Genocide, Salt Lake City, Utah: University of Utah Press, ISBN 0-87480-849-9, OCLC 61262401
- Love, Dave (Mei 1996), "The Second Battle of Ypres, April 1915", Sabretasche, 26 (4)
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Lyons, Michael J (1999), World War I: A Short History (tol. la 2nd), Prentice Hall, ISBN 0-13-020551-6
- Ludendorff, Erich (1919), My War Memories, 1914–1918, OCLC 60104290 also published by Harper as "Ludendorff's Own Story, August 1914 – November 1918: The Great War from the Siege of Liège to the Signing of the Armistice as Viewed from the Grand Headquarters of the German Army" OCLC 561160 (original title Meine Kriegserinnerungen, 1914–1918)
- Magliveras, Konstantinos D (1999), Exclusion from Participation in International Organisations: The Law and Practice behind Member States' Expulsion and Suspension of Membership, Martinus Nijhoff Publishers, ISBN 90-411-1239-1
- Martel, Gordon (2003), The Origins of the First World War, Pearson Longman, Harlow
- Mawdsley, Evan (2008), The Russian Civil War (tol. la Edinburgh), Birlinn location, ISBN 1-84341-041-9
{{citation}}
: Invalid|ref=harv
(help) - McLellan, Edwin N, The United States Marine Corps in the World War
- Meyer, Gerald J (2006), A World Undone: The Story of the Great War 1914 to 1918, Random House, ISBN 978-0-553-80354-9
- Millett, Allan Reed; Murray, Williamson (1988), Military Effectiveness, Boston: Allen Unwin, ISBN 0-04-445053-2, OCLC 220072268
- Moon, John Ellis van Courtland (Julai 1996), "United States Chemical Warfare Policy in World War II: A Captive of Coalition Policy?", The Journal of Military History, 60 (3), Society for Military History: 495–511, doi:10.2307/2944522, JSTOR 2944522
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Morton, Desmond (1992), Silent Battle: Canadian Prisoners of War in Germany, 1914–1919, Toronto: Lester Publishing, ISBN 1-895555-17-5, OCLC 29565680
- Mosier, John (2001), "Germany and the Development of Combined Arms Tactics", Myth of the Great War: How the Germans Won the Battles and How the Americans Saved the Allies, New York: Harper Collins, ISBN 0-06-019676-9
- Muller, Jerry Z (Machi–Aprili 2008), "Us and Them – The Enduring Power of Ethnic Nationalism", Foreign Affairs, Council on Foreign Relations, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Neiberg, Michael S (2005), Fighting the Great War: A Global History, Cambridge, Mass: Harvard University Press, ISBN 0-674-01696-3, OCLC 56592292
- Nicholson, Gerald WL (16 May 2007), Canadian Expeditionary Force, 1914–1919: Official History of the Canadian Army in the First World War (tol. la 1st), Ottawa: Queens Printer and Controller of Stationary, OCLC 2317262, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-16, iliwekwa mnamo 2014-07-29
{{citation}}
: Check date values in:|year=
/|date=
mismatch (help); Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Northedge, FS (1986), The League of Nations: Its Life and Times, 1920–1946, New York: Holmes & Meier, ISBN 0-7185-1316-9
- Page, Thomas Nelson, Italy and the World War, Brigham Young University, Chapter XI cites "Cf. articles signed XXX in La Revue de Deux Mondes, 1 and 15 March 1920"
- Painter, David S. (2012), "Oil and the American Century" (PDF), The Journal of American History, 99 (1): 24–39, doi:10.1093/jahist/jas073
- Phillimore, George Grenville; Bellot, Hugh HL (1919), "Treatment of Prisoners of War", Transactions of the Grotius Society, 5: 47–64, OCLC 43267276
- Pitt, Barrie (2003), 1918: The Last Act, Barnsley: Pen and Sword, ISBN 0-85052-974-3, OCLC 56468232
- Price, Alfred (1980), Aircraft versus Submarine: the Evolution of the Anti-submarine Aircraft, 1912 to 1980, London: Jane's Publishing, ISBN 0-7106-0008-9, OCLC 10324173 Deals with technical developments, including the first dipping hydrophones
- Prior, Robin (1999), The First World War, London: Cassell, ISBN 0-304-35256-X
- Raudzens, George (Oktoba 1990), "War-Winning Weapons: The Measurement of Technological Determinism in Military History", The Journal of Military History, 54 (4), Society for Military History: 403–434, doi:10.2307/1986064, JSTOR 1986064
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Repington, Charles à Court (1920), The First World War, 1914–1918, juz. la 2, London: Constable, ISBN 1-113-19764-1
- Rickard, J (5 Machi 2001), "Erich von Ludendorff, 1865–1937, German General", Military History Encyclopedia on the Web, HistoryOfWar.org, iliwekwa mnamo 6 Februari 2008
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Rickard, J (27 Agosti 2007), The Ludendorff Offensives, 21 March-18 July 1918, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-10, iliwekwa mnamo 2021-10-02
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Roden, Mike, "The Lost Generation – myth and reality", Aftermath – when the boys came home, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-01, iliwekwa mnamo 6 Novemba 2009
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Saadi, Abdul-Ilah, Dreaming of Greater Syria, Al Jazeera, iliwekwa mnamo 17 Novemba 2009
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Sachar, Howard Morley (1970), The emergence of the Middle East, 1914–1924, Allen Lane, ISBN 0-7139-0158-6, OCLC 153103197
- Salibi, Kamal Suleiman (1993), "How it all began – A concise history of Lebanon", A House of Many Mansions – the history of Lebanon reconsidered, I.B. Tauris, ISBN 1-85043-091-8, OCLC 224705916, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-04-03, iliwekwa mnamo 2014-07-29
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Schindler, J (2003), "Steamrollered in Galicia: The Austro-Hungarian Army and the Brusilov Offensive, 1916", War in History, 10 (1): 27–59, doi:10.1191/0968344503wh260oa
- Shanafelt, Gary W (1985), The secret enemy: Austria-Hungary and the German alliance, 1914–1918, East European Monographs, ISBN 978-0-88033-080-0
- Shapiro, Fred R; Epstein, Joseph (2006), The Yale Book of Quotations, Yale University Press, ISBN 0-300-10798-6
- Souter, Gavin (2000), Lion & Kangaroo: the initiation of Australia, Melbourne: Text Publishing, OCLC 222801639
- Sisemore, James D (2003), The Russo-Japanese War, Lessons Not Learned, US Army Command and General Staff College, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-04, iliwekwa mnamo 2021-01-17
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Smele, Jonathan, "War and Revolution in Russia 1914–1921", World Wars in-depth, BBC, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-11-10, iliwekwa mnamo 12 Novemba 2009
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Speed, Richard B, III (1990), Prisoners, Diplomats and the Great War: A Study in the Diplomacy of Captivity, New York: Greenwood Press, ISBN 0-313-26729-4, OCLC 20694547
{{citation}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - Stevenson, David (1996), Armaments and the Coming of War: Europe, 1904–1914, New York: Oxford University Press, ISBN 0-19-820208-3, OCLC 33079190
- Stevenson, David (2004), Cataclysm: The First World War as Political Tragedy, New York: Basic Books, ku. 560pp, ISBN 0-465-08184-3, OCLC 54001282
- Strachan, Hew (2003), The First World War: Volume I: To Arms, New York: Viking, ISBN 0-670-03295-6, OCLC 53075929
- Taylor, Alan John Percivale (1963), The First World War: An Illustrated History, Hamish Hamilton, ISBN 0-399-50260-2, OCLC 2054370
- Taylor, Alan John Percivale (1998), The First World War and its aftermath, 1914–1919, Century of Conflict, 1848–1948, London: Folio Society, OCLC 49988231
- Taylor, John M (Summer 2007), "Audacious Cruise of the Emden", The Quarterly Journal of Military History, 19 (4): 38–47, doi:10.1353/jmh.2007.0331, ISSN 0899-3718
{{citation}}
: Unknown parameter|doi_brokendate=
ignored (|doi-broken-date=
suggested) (help)CS1 maint: date and year (link) CS1 maint: date auto-translated (link) - Terraine, John (1963), Ordeal of Victory, Philadelphia: J. B. Lippincott, ku. 508pp, ISBN 0-09-068120-7, OCLC 1345833
- Tschanz, David W, Typhus fever on the Eastern front in World War I, Montana State University, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-11, iliwekwa mnamo 12 Novemba 2009
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - Tuchman, Barbara Wertheim (1966), Zimmermann Telegram (tol. la 2nd), New York: Macmillan, ISBN 0-02-620320-0, OCLC 233392415
- Tucker, Spencer C; Roberts, Priscilla Mary (2005), Encyclopedia of World War I, Santa Barbara: ABC-Clio, ISBN 1-85109-420-2, OCLC 61247250
- Tucker, Spencer C; Wood, Laura Matysek; Murphy, Justin D (1999), The European powers in the First World War: an encyclopedia, Taylor & Francis, ISBN 978-0-8153-3351-7
- von der Porten, Edward P (1969), German Navy in World War II, New York: T. Y. Crowell, ISBN 0-213-17961-X, OCLC 164543865
- Westwell, Ian (2004), World War I Day by Day, St. Paul, Minnesota: MBI Publishing, ku. 192pp, ISBN 0-7603-1937-5, OCLC 57533366
- Wilgus, William John (1931), Transporting the A. E. F. in Western Europe, 1917–1919, New York: Columbia University Press, OCLC 1161730
- Willmott, H.P. (2003), World War I, New York: Dorling Kindersley, ISBN 0-7894-9627-5, OCLC 52541937
- Winegard, Timothy, "Here at Vimy: A Retrospective – The 90th Anniversary of the Battle of Vimy Ridge", Canadian Military Journal, 8 (2)
- Winter, Denis (1983), The First of the Few: Fighter Pilots of the First World War, Penguin, ISBN 978-0-14-005256-5
- Wohl, Robert (1979), The Generation of 1914 (tol. la 3), Harvard University Press, ISBN 978-0-674-34466-2
- Zieger, Robert H (2001), America's Great War: World War I and the American experience, Lanham, Maryland: Rowman & Littlefield, uk. 50, ISBN 0-8476-9645-6
- "History in brief (Israel)", The Economist, 28 Julai 2005, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Israeli Foreign Ministry, Ottoman Rule, Jewish Virtual Library, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
- A multimedia history of World War I
- The Heritage of the Great War/ First World War. Graphic color photos, pictures and music, Netherlands
- The World War I Document Archive Wiki, Brigham Young University
- Maps of Europe Ilihifadhiwa 5 Julai 2014 kwenye Wayback Machine. covering the history of World War I at omniatlas.com
- Your Family History of World War I – Europeana 1914–1918(Crowd-sourcing project)
- EFG1914 – Film digitisation project on First World War
- WWI Films on the European Film Gateway
- World War I British press photograph collection – A sampling of images distributed by the British government during the war to diplomats overseas, from the UBC Library Digital Collections
- The British Pathé WW1 Film Archive Ilihifadhiwa 24 Machi 2019 kwenye Wayback Machine.
Ramani hai
- An animated map "Europe plunges into war" Ilihifadhiwa 4 Juni 2020 kwenye Wayback Machine.
- An animated map of Europe at the end of the war Ilihifadhiwa 4 Juni 2020 kwenye Wayback Machine.