Ufashisti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fascio Littorio, ishara ya ufashisti iliyoupatia jina.
Benito Mussolini na Adolf Hitler, viongozi wa ufashisti katika Ulaya.

Ufashisti ni siasa ya mrengo wa kulia ambayo ilitawala Italia tangu mwaka 1922 hadi 1943 ikiongozwa na mwanzilishi wake, dikteta Benito Mussolini (1883-1945).

Kutokana nayo, aina za siasa zinazofanana zinaitwa pia ufashisti. Nchi nyingine ambako siasa ya kifashisti ilitawala, zilikuwa pamoja na Ujerumani chini ya Adolf Hitler na kwa kiasi kidogo pia Hispania chini ya Francisco Franco. Ufashisti ulienea hasa Ulaya katika nusu ya kwanza ya karne ya 20.

Tabia za ufashisti ni uzalendo mkali, utawala wa kidikteta, ukandamizaji wa upinzani wote, na majaribio ya kuathiri sehemu zote za jamii na pia za uchumi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]