Redio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Redio mnamo 1950
Redio mnamo 2000

Redio (au rungoya) ni chombo (kifaa) kinachopokea mawasiliano kutoka katika kituo cha redio na kuyabadilisha kuwa sauti.

Kwa kawaida rungoya inapokea kwa njia ya antena yake mawimbi sumakuumeme yanayosambazwa na antena ya kituo cha rungoya. Kuna pia aina za rungoya ambako mawasiliano hufika kwa umbo la alama za umeme katika waya. Mawasiliano ya sumakuumeme yanasambazwa pia kwa njia ya chomboanga au satelaiti lakini njia hii inahitaji vyombo maalumu na antena ya kawaida haitoshi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1886 Mjerumani Heinrich Hertz alitambua mawimbi ya sumakuumeme. Wataalamu na muhandisi mbalimbali walifanya majaribio katika miaka iliyofuata kutumia mawimbi haya kwa mawasiliano, kati yao Mwitalia Guglielmo Marconi, Mmarekani Nikola Tesla na Mrusi Alexander Popov. Kila mmoja ametajwa kama "mtu wa kwanza aliyegundua rungoya".

Kituo cha kwanza cha rungoya kilianzishwa na Mholanzi Hanso Schotanus à Steringa Idzerda tarehe 6 Novemba 1919 aliposambaza muziki kutoka nyumba yake. Kituo cha kwanza cha kibiashara kilianza kazi mwaka 1920 Marekani mjini Pittsburgh.

Katika miaka iliyofuata redio ilisambaa kote duniani. Ni njia muhimu ya kusambaza habari pamoja na utamaduni, hasa muziki.

Matumizi ya redio[hariri | hariri chanzo]

Hapo zamani, redio zilitumika na mabaharia kwa kutuma jumbe toka chombo majini hadi nchi kavu kwa kutumia kodi za Morsi (Morse code). Wakati chombo kilichojulikana kama Titanic kilikuwa kinazama mwaka 1912, jumbe zilitumwa kutoka kwa mabaharia waliokuwa kwenye chombo hicho kwa vyombo vilivyokuwa karibu.

Wanajeshi pia walitumia redio kutuma jumbe na kuwasiliana na makao yao makuu.

Leo, redio hutumika kwa mawasiliano, matangazo na muziki. Kabla ya uvumbuzi wa televisheni, redio zilitumika kwa uigizaji na vichekesho. Redio za leo zinatumia wavu za dijitali na huweza kushika wavu kwa urahisi zaidi.

Pia kuna redio za kushikwa kwa mikono [1].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]