Simu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Simu ya zamani.
Simu za kisasa.

Simu (kutoka Kiarabu سیم, sim, inayomaanisha "waya") ni chombo cha mawasilianoanga kinachotumia umeme.

Matumizi ya simu ni kwa ajili ya watu wawili walio katika sehemu mbili tofauti kuongea.

Awali simu ilihitaji iunganishwe na nyaya, lakini leo hii inaweza kutumia redio. Hiyo inaitwa nyayatupu, siwaya au simu bila waya.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Watu wengi wanaamini kuwa simu iligunduliwa mnamo 1876 na Alexander Graham Bell,[1] Mskoti mwenye umri wa miaka 29 aliyeishi nchini Marekani. Lakini Mwitalia Antonio Meucci alianzisha matumizi ya simu toka mwaka wa 1871 hukohuko Marekani.

Tangu mwishoni mwa karne ya 20 kuna aina mpya ya simu iliyoenea ambayo ni simu ya mkononi. Ingawa haistahili kweli kuitwa tena "simu" kwa maana asilia kwa sababu hakuna simu, ni aina ya mtambo wa mawasiliano uliosambaa haraka sana.

Katika nchi nyingi za Afrika simu hizi zina faida ya pekee kwa sababu zinaruhusu mawasiliano hata pale ambako nyaya za Posta hazifiki.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Alexander Graham Bell Laboratory Notebook, 1875-1876 (1875-1876). Iliwekwa mnamo 2013-07-23.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]