Ugiriki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ugiriki

Ugiriki (pia: Uyunani; kwa Kigiriki cha kisasa: Ελλάδα, Ellada, au Ελλάς, Ellas) ni nchi ya Ulaya Kusini-Mashariki iliyopo kusini mwa rasi ya Balkani.

Imepakana na Albania, Masedonia Kaskazini, Bulgaria na Uturuki. Upande wa kusini-magharibi na kusini-mashariki kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Mediteranea.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kijiografia huwa na sehemu za Ugiriki bara, rasi ya Peloponesi upande wa kusini inayounganishwa kwa shingo ya nchi nyembamba, halafu visiwa vingi upande wa Bahari ya Aegean, Bahari ya Adria na kwenye Mediteranea yenyewe. Visiwa vikubwa zaidi ni Kreta, Euboea, Lesbo na Rhodos.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Parthenon, katika Akropoli ya Athens, ni kielelezo cha Ugiriki wa Kale.

Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu na maarufu sana, hata inaitwa "nchi mama ya Ulaya" na kitovu cha Ustaarabu wa magharibi, kwa sababu ndipo vilipoanza demokrasia, falsafa ya magharibi, fasihi ya magharibi, historiografia, sayansi ya siasa, tafiti za sayansi na hisabati, tamthilia na michezo ya Olimpiki.

Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kigiriki inaendelea kuandikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki inayotumiwa tangu miaka 3000 iliyopita, lakini lugha yenyewe imebadilika. Wagiriki wa leo hawaelewi tena Kigiriki cha Kale moja kwa moja.

Wakazi wengi wanafuata dini ya Ukristo (93%), hasa katika Kanisa la Kiorthodoksi la Kigiriki (90%), halafu Waprotestanti na Wakatoliki. 2% ni Waislamu.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ugiriki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.