Nenda kwa yaliyomo

Serbia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Serbia
Република Србија
Republika Srbija
Wimbo wa taifa: "Боже правде"
Bože pravde
("Mungu wa Haki")
Mji mkuu
na mkubwa
Belgrade
Lugha rasmiKiserbia
Dini (2022)
UraiaMserbia
SerikaliJamhuri ya bunge ya umoja
  Rais
Aleksandar Vučić
  Waziri Mkuu
Đuro Macut
Historia ya kuundwa
  Ufalme wa Serbia (mwanzo)
Karne ya 7
  Ufalme wa Serbia
1217
Eneo
  Jumlakm2 88,499
Idadi ya watu
  Kadirio la 20256,567,783
PLT (PPP)Kadirio la 2026
  Jumla$225.55 bilioni
  Kwa kila mtu$34,790
PLT (Kawaida)Kadirio la 2026
  Jumla$112.11 bilioni
  Kwa kila mtu$17,290
HDI (2023)0.833 juu sana
Gini (2025)32.0
SarafuDinar ya Serbia
Majira ya saaUTC+1
Msimbo wa simu++381
Jina la kikoa.rs .срб
Tanbihi:
1 Jimboni Vojvodina zifuatazo ni lugha rasmi kieneo: Kihungaria, Kislovakia, Kiromania, Kirusyn na Kikroatia. Katiba mpya imepanga pia kukubaliwa kwa mwandiko wa Kilatini kwa Kiserbia pamoja kisirili. Jimboni Kosovo lugha rasmi ni pia Kialbania na Kiingereza.
2 Euro hutumiwa jimboni Kosovo pamoja na dinar.
3 ".rs" ni rasmi tangu Septemba 2006 lakini anwani zenye ".yu" bado zinatumiwa.
4 pamoja na Montenegro hadi 2007.

Serbia (kwa Kiserbokroatia: Република Србија au Republika Srbija) ni nchi isiyo na pwani iliyoko Kusini-Mashariki mwa Ulaya, kwenye rasi ya Balkani. Imepakana na Hungaria, Bulgaria, Romania, Masedonia Kaskazini, Kosovo (au Albania), Montenegro, Bosnia na Herzegovina na Kroatia. Ina idadi ya watu takriban milioni 6.5 huku Belgrad ukiwa mji mkuu na mji mkubwa, wenye wakazi milioni 1.2. Lugha rasmi Kiserbia.

Serbia inaendeshwa kama jamhuri ya bunge yenye mfumo wa vyama vingi vya kisiasa. Serbia ina uchumi unaoendelea wa kipato cha juu cha kati, unaotegemea kilimo, viwanda, nishati, pamoja na sekta ya huduma na teknolojia inayokua. Huzalisha mazao kama ngano, mahindi, na matunda, na ina viwanda muhimu katika utengenezaji wa magari, uchimbaji madini, na uzalishaji wa nishati. Serbia pia ni mgombea wa kujiunga na Umoja wa Ulaya na inaendeleza uhusiano wa kiuchumi na kisiasa na nchi za Magharibi pamoja na mataifa kama Urusi na China. Licha ya maendeleo yaliyopatikana, inakabiliwa na changamoto kama mageuzi ya kiuchumi, kupungua kwa idadi ya watu, na masuala ya kisiasa yanayohusiana na hadhi ya Kosovo.

Kiutamaduni, Serbia ina urithi tajiri ulioundwa na karne nyingi za ushawishi kutoka Dola la Bisanti , Ottoman, na Austro-Hungaria. Idadi kubwa ya watu hufuata Ukristo wa Uorthodoksi wa Mashariki, ambao una nafasi muhimu katika utambulisho wa taifa, mila, na sikukuu. Lugha ya Kiserbia hutumia alfabeti za Kikirili na Kilatini. Nchi hii inajulikana kwa mchango wake katika fasihi, muziki, michezo, na sayansi, pamoja na historia yake.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Waslavi walihamia Balkani baada ya karne ya 6.

Kati yao, Waserbia waliunda falme mbalimbali mwanzoni mwa Karne za Kati.

Mwaka 1217 Ufalme wa Serbia ulitambuliwa na Roma na Bizanti na mwaka 1346 ulifikia kilele cha ustawi wake kama Dola la Serbia.

Hali hiyo haikudumu muda mrefu, tena katikati ya karne ya 16 eneo lote la Serbia ya leo lilitekwa na Waosmani, ingawa wakati mwingine sehemu yake ilitawaliwa na Dola la Wahabsburg.

Mwanzoni mwa karne ya 19, mapinduzi ya Serbia ilileta ufalme wa kikatiba wa kwanza katika Balkani.

Ufalme huo ulizidi kuenea na baada ya vita vikuu vya kwanza vilivyosababisha vifo vingi vya raia zake, Serbia iliungana na makabila kuanzisha Yugoslavia iliyodumu hadi miaka ya 1990 iliposambaratika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 2006 hata Montenegro ilitengana na Serbia, ila kwa amani.

Mwaka 2008 bunge la jimbo la Kosovo lilijitangazia uhuru.

Demografia

[hariri | hariri chanzo]

Nchi, ukiondoa Kosovo, ina wakazi 6,567,783 kwenye eneo la km² 88,499. Wengi wao wana asili ya Kislavoni, lakini 2.8% wana asili ya Hungaria, 2% ni Waromani, n.k.

Upande wa dini 81.1% ni Waorthodoksi, 3.9% Wakatoliki, 1.7% Wakristo wengine, 4.2% Waislamu.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Serbia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.