Dizeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Diseli)
Rukia: urambazaji, tafuta

Dizeli ni fueli inayofaa kuendesha injini ya diseli. Kwa kawaida inapatikana kwa njia ya mvewevusho wa mafuta ya petroli lakini kuna pia fueli zenye tabia za dizeli zinazotengenezwa kwa kutumia mafuta kutokana na biomasi ya mimea au mbegu za mimea na hii ni aina ya biofueli.

Jina la dizeli ni kumbukumbu ya mhandisi Mjerumani Rudolf Diesel aliyebuni injini maalumu.

Dizeli ya kawaida hutengenezwa kwa njia ileile kama petroli kutokana na mafuta ya petroli kwa njia ya mvevusho; ila tu diseli ni sehemu ile inayotoka baada ya petroli kama halijoto cha mafuta yanayochemshwa yanazidi sentigredi 200. Mafuta hupashwa moto hadi dutu mbalimbali ndani yake hufikia kiwango cha kuchemka na kuwa gesi. Petroli ni nyepesi na kutangulia halafu zinafuata mafuta ya taa na diseli.

Kwa ajili ya matumizi ya injini mbalimbali matokeo ya mwevusho yanachanganywa na kukorogwa kwa shabaha ya kupata diseli sanifu; mafuta asilia hutofautiana kikemia kwa hiyo viwango vya viowevu vyepesi na vizitoa vinavyopatikana katika mvweusho vinatofautinana kila mara.

Injini za dizeli ni kubwa na nzito zaidi kuliko injini za petroli kwa hiyo zinatumiwa zaidi kwa malori, mabasi au kwenye meli. Hii ni sababu ya kwamba katika nchi nyingi diseli huuzwa kwa bei nafuu kwa sababu serikali inataka kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa zinazobebwa na malori hasa. Lakini katika nchi kadhaa kuna pia motokaa ndogo ya abiria yenye injini za diseli; hata kama bei ya injini ya diseli inapaswa kuwa kubwa kiasi kuliko injini ya petroli ole bei nafuu ya fueli hii inasababisha watu wengi kutafuta magari yenye injini ya diseli.