Mafuta ya petroli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Chupa cha mafuta ya petroli; chupa chenyewe ni cha plastiki inayotengenezwa na mafuta hii
Pampu ya mafuta ya petroli

Mafuta ya petroli (pia petroliamu kutoka Kigiriki petros = mwamba na Kilatini oleom = mafuta) ni kiowevu kinene chenye rangi cheusi hadi kijani. Inatokea kiasili katika ardhi na inawaka rahisi. Ni chanzo cha petroli, fueli mbalimbali, madawa mengi na plastiki. Ni kati ya vyanzo muhimu kabisa vya nishati vinavyoshughulikiwa na binadamu kama fueli ya usafiri na ya kutengeneza umeme.

Kikemia mafuta ya petroli ni mchanganyiko wa dutu hasa hidrokaboni mbalimbali. Inatumiwa kwa njia ya mwevusho ikipashwa na moto na sehemu zake kutenganishwa zikifikia kiwango cha kuchemka kwa nyakati mbalimbali.

Chanzo cha mafuta ya petroli[hariri | hariri chanzo]

Petroliamu hupatikana ndani ya maganda ya mwamba. Wataalamu wengi hukubaliana ya kwamba iliundwa baharini. Maji ya bahari yanajaa algae na planktoni inayoishi kutokana na uwezo wake wa usanisinuru. Viumbe hivi vidogo vinakufa na kuzama chini katika vilindi vya bahari vikifunika tako la bahari kama ganda. Katika kina kikubwa ya mita mielfu mabaki yale hayawezi kuoza kutokana na uhaba wa oksijeni yanageukia kuwa ganda la matope.

Kila baada muda mashapo mineralia (kama vile mchanga, vumbi ya hewani) yanashuka pia hadi tako la bahari na kufunika matope yaliyotokea na planktoni. Maganda yale ya mashapo mineralia yanawezakuwa manene na mazito hadi yanaanza kukandamiza tope na kuisababisha kuwa moto. Katika mazingira ya shindikizo na joto molekuli ndefu za hidrati kabonia za biomasi zinavunjwa kuwa molekuli fupi katika mchakato unaoigwa na teknolojia ya mvevusho.

Molekuli hizi fupi zinatembea katika vinyweleo ndani ya mwamba ya mashapo hadi kufikia aina ya mwamba penye nafasi ndogondogo ambako molekuli nzito zakusanya kama petroliamu na molekuli nyepesi sana kama gesi asilia. Kama kuna ganda la mwamba imara lililopo juu ya mwamba vinyweleo akiba ya petroliamu na gesi inaanza kutokea na mara nyingi molekuli nyepesi za gesi huwa kama "kofia" ya gesi asilia juu ya "ziwa" la petroliamu. Hii ni sababu ya kwamba mara nyingi gesi asilia inapatikana pamoja na petroliamu.

Historia ya matumizi yake[hariri | hariri chanzo]

Tangu nyakati za kale mafuta ya petroli ilitokea kiasili kutoka ardhi katika nchi kama Mesopotamia kusini. Pale ilipoonekana kama ziwa iliunganika na oksijeni ya hewa na kuganda kuwa lami. Ile lami asilia iliwahi kutumiwa na watu wa kale; kwa kuikoroga na mchanga watu waliweza kuziba mapengo kati ya bao za jahazi.

Pia wenyeji wa Babeli walimwaga tayari mafuta ya petroli asilia juu ya barabara za udongo shauri la kuimarisha uso wake.

Baadaye Waroma na Wabizanti walitumia mafuta hii kama silaha za kumwaga moto dhidi ya maadui hasa baharini.

Lami na mafuta ya petroli zilitumiwa pia kama madawa ya tiba kwa maradhi mbalimbali.

Wakati wa karne ya 19 daktari Mkanada Abraham Gesner aligundua ya kwamba alliweza kutengeneza mafuta ya taa kutoka kwa mafuta haya. Hadi wakati ule ni hasa mafuta ya nyangumi yaliyotumiwa kama mafuta ya taa lakini ilizidi kuwa ghali. Mafuta mpya yalipokelewa haraka yalipatikana kwa bei nafuu na katika nchi nyingi watu walianza kutafuta chemchemi asilia za mafuta ya petroli.

Wakati wa mwisho wa karne ya 19 Carl Benz alibuni motokaa iliyotumia injini ya mwako wa ndani kwa kutumia petroli. Kutokana na juhudi za Henry Ford za kujenga motokaa kwa bei ndogo mahitaji ya petroli yaliongezeka tena.

Usambazaji wa motokaa ulisababisha kuzalishwa kwa petroli kwa wingi na haja la kukwa na mafuta ya petroli kuongezeka.

Uzalishaji wa petroliamu[hariri | hariri chanzo]

Jedwali inayofuata inaorodhesha nchi ambako petroliamu hutolewa ardhini kufuatana na uwingi wa uzalishaji.

Kipimo cha uwingi ni kiasi cha mapipa kwa siku (Kiingereza "barrels per day" - kifupi "bbl/d").

# Nchi ya kuzalisha mafuta ya petroli 1,000 bbl/d (2006) 1,000 bbl/d (2007) 1,000 bbl/d (2008) 1,000 bbl/d (2009) Asilimia ya uzalishaji duniani
mwaka 2009
1 Saudia 10,665 10,234 10,782 9,760 11.8%
2 Urusi 1 9,677 9,876 9,789 9,934 12.0%
3 marekani 1 8,331 8,481 8,514 9,141 11.1%
4 Uajemi (OPEC) 4,148 4,043 4,174 4,177 5.1%
5 China 3,845 3,901 3,973 3,996 4.8%
6 Kanada 2 3,288 3,358 3,350 3,294 4.0%
7 Mexico 1 3,707 3,501 3,185 3,001 3.6%
8 Falme za Kiarabu (OPEC) 2,945 2,948 3,046 2,795 3.4%
9 Kuwait (OPEC) 2,675 2,613 2,742 2,496 3.0%
10 Venezuela (OPEC) 1 2,803 2,667 2,643 2,471 3.0%
11 Norwei 1 2,786 2,565 2,466 2,350 2.8%
12 Brazil 2,166 2,279 2,401 2,577 3.1%
13 Iraq (OPEC) 3 2,008 2,094 2,385 2,400 2.9%
14 Algeria (OPEC) 2,122 2,173 2,179 2,126 2.6%
15 Nigeria (OPEC) 2,443 2,352 2,169 2,211 2.7%
16 Angola (OPEC) 1,435 1,769 2,014 1,948 2.4%
17 Libya (OPEC) 1,809 1,845 1,875 1,789 2.2%
18 Ufalme wa Maungano
(Uingereza na Uskoti)
1,689 1,690 1,584 1,422 1.7%
19 Kazakhstan 1,388 1,445 1,429 1,540 1.9%
20 Qatar (OPEC) 1,141 1,136 1,207 1,213 1.5%
21 Indonesia 1,102 1,044 1,051 1,023 1.2%
22 Uhindi 854 881 884 877 1.1%
23 Azerbaijan 648 850 875 1,012 1.2%
24 Argentina 802 791 792 794 1.0%
25 Oman 743 714 761 816 1.0%
26 Malaysia 729 703 727 693 0.8%
27 Misri 667 664 631 678 0.8%
28 Kolombia 544 543 601 686 0.8%
29 Australia 552 595 586 588 0.7%
30 Ecuador (OPEC) 536 512 505 485 0.6%
31 Sudan 380 466 480 486 0.6%
32 Syria 449 446 426 400 0.5%
33 Guinea ya Ikweta 386 400 359 346 0.4%
34 Thailand 334 349 361 339 0.4%
35 Vietnam 362 352 314 346 0.4%
36 Yemen 377 361 300 287 0.3%
37 Denmark 344 314 289 262 0.3%
38 Gabon 237 244 248 242 0.3%
39 Afrika Kusini 204 199 195 192 0.2%
40 Turkmenistan (hakuna takwimu) 180 189 198 0.2%

Chanzo: U.S. Energy Information Administration

1 Uzallishaji wa mafuta umeshapita kilele chake katika nchi hii kutokana na jumla ya akiba zake.

2 Uzalishaji kutokana na akiba za kawaida unapungua katika Kanada, lakini uzalishaji kutokana na mchanga mwenye mafuta unaongezeka; pamoja na mafuta yaliyopo ndani ya mchanga akiba za Kanada ni kubwa dunani baada ya Saudia.

3 Iraki ni mwanachama wa OPEC lakini uzalishaji wake haukuhesabiwa katika takwimu za OPEC tangu 1998.


Matatizo ya matumizi ya petroliamu[hariri | hariri chanzo]

Petroliamu ni fueli yenye faida nyingi; inatolewa ardhini rahisi, insafirishwa haraka na kuwa na nafasi nyingi za kuitumia kwa manufa ya kibinadamu. Ilikuwa fueli iliyowezesha maendeleo ya kiuchumi ya karne ya 20.

Siki hizi kuna wasiwasi nyingi kuhusu matumizi yake ya fueli kwa sababu ni fueli kisukuu maana ikitumiwa haiongezeki tena wala kurudi ilionekana ya kwamba akiba zake zitaishia siku moja. Hapa wasiwasi kubwa ni ya kwamba uchumi wa dunia umejengwa juu ya msingi unaoendelea kufifia na kuna hatari ya kwamba uchumi unapata mshtuko mkubwa kama akiba za mafuta ya petroli zinaendelea kupungua na bei zake kupanda.

Vilevile matumizi yake inatoa gesi nyingi hewani amabazo zinaleta hasara kwa mazingira hasa gesi ya dioksidi kabonia inayochangia kwenye kupanda kwa joto duniani kwenye hatari nyingi.

Hapo ndipo sababu kuu za utafiti mwingi kugundua vyanzo vya nishati mbadala.

Kurasa nyingine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Jina la kiungo