Nenda kwa yaliyomo

Nyeusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Puto juu ya theluji: Puto haiakisii nuru hivyo inaonekana nyeusi; theluji chini yake inaakisi sehemu zote za nuru hivyo inaonekane nyeupe.

Nyeusi ni rangi tunayoona wakati jicho letu halipokei nuru, au miale ya nuru hafifu sana.

Hapa ni sababu wengine husema nyeusi si rangi bali uhaba wa rangi zote.

Kifizikia gimba lolote huonekana jeusi, kama haliakisii nuru hata kidogo.

Nyeusi ni rangi na makaa, ya usiku na ya giza. Kinyume chake ni nyeupe.

Katika tamaduni mbalimbali imepewa maana tofauti; mara nyingi ya huzuni (kama watu wanaofiwa wanaaa mavazi meusi). Katika uamaduni wa Ulaya ilikuwa pia rangi ya mamlaka na heshima kwa hiyo majaji na wachungaji wanaweza kuvaa gauni nyeusi, pia wanaume kuvaa suti nyeusi kwa nafasi maalumu.