Mwanaume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Michelangelo alichonga katika marumaru sanamu ya Daudi kama kielelezo cha umbile la mwanamume.

Mwanaume (pia: mwanamume) ni binadamu wa jinsia ya kiume. Kwa kawaida ni mtu mzima anayeitwa hivi, kwani wanaume wadogo huitwa watoto wa kiume tu au wavulana.

Wanaume ni takriban nusu ya binadamu, wengine huwa wanawake. Wanaume na wanawake ni jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.

Kuna tabia za pekee katika maumbile ya mwili. Wanaume huwa na viungo vya uzazi vya kiume ambavyo ni pekee kama vile mboo (uume, dhahakari) na mapumbu (korodani).

Wakati wa kubalehe homoni ya testosteroni inaongezeka mwilini mwa mwanaume na kusababisha tabia kama sauti ya chini, kongezeka ya nywele mwilini (kwa mfano ndevu), kuongezeka kwa upana wa mabega na kiwango cha musuli mwilini kulingana na wanawake.

Msingi wa tofauti hizo ni hasa chembeuzi kinachoitwa "Y" yaani wanaume wana jozi la chembeuzi "X" na "Y" ndani ya seli zao zote, lakini wanawake wana jozi la "X" mbili. Chembeuzi Y inabeba habari zote zinazomfanya mwanadamu kukua kama mwanaume badala ya mwanamke.

Lakini si tofauti za mwilini pekee zinazosababisha wanaume kuwa tofauti na wanawake. Kuna pia tabia za kiakili na za kiroho za pekee zinazoonekana kati ya wanaume wengi.

Hata hivyo tofauti nyingi zinategemea pia utamaduni kwa sababu mara nyingi watu wamepanga shughuli na pia namna ya maisha tofauti kwa wanaume na wanawake, hivyo watu wamezoea kuchukua matokeo ya mapatano haya kama jambo la kimaumbile hata kama ni la kiutamaduni tu.

Pamoja na hayo, kuna wanaume wasio wachache sana wenye tabia zinazotazamiwa kuwa za kike kwa sababu miili yao huwa na viwango tofauti za homoni kama testosteroni na estrogeni. Kuna watu kadhaa wenye mwili wa kiume wanaojisikia kuwa wanawake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Andrew Perchuk, Simon Watney, Bell Hooks, The Masculine Masquerade: Masculinity and Representation, MIT Press 1995
  • Pierre Bourdieu, Masculine Domination, Paperback Edition, Stanford University Press 2001
  • Robert W. Connell, Masculinities, Cambridge : Polity Press, 1995
  • Warren Farrell, The Myth of Male Power Berkley Trade, 1993 ISBN 0-425-18144-8
  • Michael Kimmel (ed.), Robert W. Connell (ed.), Jeff Hearn (ed.), Handbook of Studies on Men and Masculinities, Sage Publications 2004

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Men


People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanaume kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.